Waliokosa mkopo waandamana dar

Waliokosa mkopo waandamana dar

Katabalo

Senior Member
Joined
Mar 29, 2011
Posts
115
Reaction score
14

[TD="bgcolor: #ffffff"] ZAIDI ya wanafunzi 50 waliochaguliwa kujiunga katika vyuo vikuu mbalimbali nchini kwa mwaka huu, jana waliandamana kwenda Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, kwa lengo la kukutana na Waziri Shukuru Kawambwa, baada ya kukosa mikopo.
Wakizungumza na Tanzania Daima Jumatano, wanafunzi hao walisema zaidi ya wanafunzi 200 wenye sifa za kupewa mikopo ya elimu na Bodi ya Mikopo (HELBS), wamenyimwa bila maelezo.
Walisema kuwa tangu mwisho wa wiki wamekuwa wakihangaika kujua sababu za kutopewa mikopo kutoka katika bodi hiyo bila mafanikio.
Mwanafunzi Ayoub Suleiman aliyechaguliwa katika Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), alisema kuwa wameamua kumfuata Waziri Kawambwa ili wajue ni kwa nini hawajapewa mikopo hiyo.
Alisema majibu ya wanafunzi walioomba mikopo hiyo yalitoka Septemba 27 mwaka huu, miongoni mwao hawakuwepo kwa maelezo kuwa bajeti imekwisha.
“Waliotupa majibu haya ni wafanyakazi wa mapokezi na walinzi pale bodi ya mikopo, sio wahusika wenyewe kwa kuwa kila tulipoomba kukutana na mkurugenzi, hatukupata nafasi hiyo,” alisema Suleiman.
Mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Mzumbe, Godwin Uledi, alisema kuwa juzi waliwashuhudia baadhi ya wazazi wakiwa na suti na magari ya kifahari wakifika kwenye ofisi za bodi hiyo na watoto wao, na kuingia moja kwa moja kuonana na watendaji, walipotoka walikuwa wakitabasamu, hali iliyoonyesha kuwa wamefanikiwa.
Alisema, wanataka wapewe sababu kwa nini hawajapewa mikopo ilhali wenzao wenye vigezo kama vyao wamepata?
“Taasisi ya vyuo vikuu nchini ‘TCU’ ilitoa mwongozo kuwa wanafunzi wanaotarajia kujiunga na vyuo vikuu wakiomba vitivo vya elimu, uhandisi, udaktari, kilimo na sayansi watapata kipaumbele katika mikopo, hivyo nasi tulifuata mwongozo huo ili tupewe mikopo lakini hatujafanikiwa.
“Isingekuwa tunahitaji mikopo hii tungeomba katika maeneo mengine ambayo tulikuwa tukikidhi vigezo. Tumeomba katika vitivo hivi ili tupate mikopo,” alisema.
Kwa upande wake mwanafunzi aliyechaguliwa katika Chuo Kikuu cha Mt. Augustine, Revocatus Baltazary, alisema kuwa wamefungua chuo tokea Septemba 18, lakini ameshindwa kuripoti kutokana na wazazi wake kuwa na kipato cha chini.
“Sasa sina hata kianzio cha kwendea huko, kwa kuwa wazazi wangu hawana uwezo nitakwendaje?,” alihoji.
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano, Ntambi Bunyazu, alisema kuwa wizara imewasiliana na bodi ya mikopo, kwamba wanafunzi hao warudi kule wakapewe maelezo zaidi kwa kuwa kila mmoja ana tatizo lake.
Hadi Tanzania Daima Jumatano inaondoka katika maeneo hayo, wanafunzi hao waliambiwa waorodheshe tena majina ili wizara iyapeleke HELBS, baada ya wiki moja watakuwa wamepata majibu.
Jitihada za kumtafuta Mkurugenzi Msaidizi wa Habari, Elimu na Mawasiliano wa HELBS, Cosmas Mwaisobya, kwa ajili ya ufafanuzi wa suala hilo, ziligonga mwamba baada ya simu yake ya kiganjani kuita kwa muda mrefu bila majibu.


[TD="bgcolor: #ffffff"]
TANZANIA DAIMA,LEO OCT 2, 2013

Wanafunzi waandamana Dar



na Lucy Ngowi


[/TD]
[TD="width: 200, bgcolor: #FFFFFF, align: center"]


[/TD]
[/TD]
sOURCE: TANZANIA DAIMA
 
Nipo ukonga makao makuu ya f f U wanafanya mazoezi sijui ya nini ? Leo kauli ya pinda lazima itimie wapigwe tu
 
Tumechoka kuonewa nawaunga mkono na mie nlikuwepo japo nmepata mkopo.
 
Kweli ndugu.. me mwenyewe ni victim kwenye hii issue. Hasa sisi tuliopitia diploma ndo kabisaa hawajatufikiria
 
Nipo ukonga makao makuu ya f f U wanafanya mazoezi sijui ya nini ? Leo kauli ya pinda lazima itimie wapigwe tu

Ahahahaa. Tuko fiti baada ya Jkt. Hata Ak47 tunajua kuzitumia. SMG tumecheza nazo. Sasa wakitaka tifu litatokea tu labda watuletee kaka zetu JWTZ. Ijumaa naisubiria kwa hamu sana! BACK TO HESLB MOVEMENT
 
wahusika wazipoziba ufa mda huu kabla ya vyuo kufunguliwa sijui kama hawa walionza kuandamana leo watatulia wakiwa chuo.mwishowe mtakuja kusingizia chadema
 
Waandamane tu hela zipo, wanatafuta jinsi ya kukopesha majina vivuli, ya watu wasiokuwepo na waliokufa ili wakaongezee hizo pesa kwenye account zao za uswizi
 
Vijana msirudi nyuma mpaka kieleweke! Ikibidi mtinge mpaka ikulu. Ila mwandishi wa TD ni kanjanja, yaani HESLB anaandika HELBS (Higher Education Loans Board Students)? Au jamaa anatafsiri yake ya hiyo bodi?
 
Haiwezekani kamwe kukaa katika nchi ambayo baadhi ya watu ni secured na wengine sio secured bora tufanye vurugu vyuo vifungwe mpaka hapo fursa sawa kwa wote itakapopatikana.no loan no studies! By ant-secured
 
xa me cjamuelewe eti waandike majina yao hlf watapata mjib baada ya wk moja, je ambaye yupo mtwara au kigoma na yeye aandike jina lake wapi?
 
Wamezoea sana mtelemko kuchukua pesa za wanaoitaj na kwenda kuzitunza tu kwenye account zao ila dis time wamechemsha..............tusitulie hadi kieleweke ------- zao
 
Hela zipo watoto wa matajiri hawakosi mkopo kwann
 
Back
Top Bottom