Habari yako kiongozi? Mara nyingi haya madai hulipwa ndani ya wiki sita kama documents zote zipo na hazina shaka, na kila hatua jinsi faili linavyoshughulikiwa kama umejiunga na huduma ya NSSF online unakuwa unaona kipi kinachoendelea na mpaka faili likiwa APPROVED na siku ya kulipwa pia inaonekana. Vilevile ukishaingia hapo kwenye USER-PORTAL upande wa STATUS kwa kipengele cha CLAIMS DETAILS ukiona wameweka neno LODGING hapo ujuwe faili lako limeanza kufanyiwa kazi. Likitoka kuwa LODGING linakuja kuwa APPROVED baada ya hapo inakuwa PAID. Usivunjike moyo Kiongozi pesa yako utaipata tu kwani si walikupa tarehe ya kurudi tena iwapo pesa yako itakuwa bado haijaingia kwenye akaunti? Mara nyingi huwa ni kipindi cha matazamio cha miezi miwili, lakini hiyo miezi miwili huwa haifiki inacheza kwenye wiki sita hadi saba. Endelea kuwa na subira kiongozi, nakutakia siku njema.