Mwaka 2007 ulikuwa ni highest peak kwa ufaulu na baada ya hapo mambo yalianza kuvurugika sana, mambo mengi yanachangia.
1. Walio maliza 2008 kama mnakumbuka walivurugwa na Mungai (hawa ni watu wa physics with chemistry.
2. Watu wa 2009 hawa hawakuwa na mtihani wa form two, wasiojiweza wengi walifika form four.
3. 2010 kulikuwa na uchaguzi wa kitaifa, kila mtu alikuwa bize na siasa, kama mnakumbuka mwaka huu nia halisi ya mgomo wa walimu ili wapandishiwe mshahara ilionekana.
4. Mwaka 2010 pia watoto walilipiwa ada ya mtihani na serikali, kwa hiyo ni lazima serikali ifanye kila linalo wezekana.
5. Mwaka 2011 hawa watoto pia hawakuwa na mtihani wa form two, na mgomo baridi wa walim uliendelea kushika kasi.
6. Mwaka 2012 mgomo wa walimu uliingia hadi vijijini na kuanza kuingia mioyoni mwa walimu na mwaka huo huo kulikuwa na mgomo dhahili wa walimu japokuwa ulikatizwa.
7. 2012 huu mwaka licha ya kuwa na mgomo dhahili wa walimu, pia mwaka huu kulikuwa na sensa iliyo chukua mwezi mzima, what do you expect from these two?
8. Mwaka 2013 up to date mgomo wa walimu (mgomo baridi) umeingia uvunguni mwa mioyo ya walimu, na hivi sasa nao wamefunga EFD/LUKU kwenye ufundishaji siku hizi walimu wanasema FUNDISHA KADRI UNAVYO LIPWA (FUKU).
9. Kuna sababu zingine nyingi, kama miundombinu mibovu, mazingira yasiyo rafiki katika ufundishaji, na nyingine nyingi.
10. Slogani mpya ya serikali ya "SIASA KWANZA ELIMU BAADAE" nayo imechangia kwa kiasi kikubwa, kusema kweli wakuu wa shule wanapata tabu sana na hawa watu waitwao madiwani.
Mie ni hayo tu wandugu, i stdand to be corrected.
Rudi kwenye analysis yako seems huna data na kinachokusumbua ni ushabiki. Nakusaidia, mimi nimemaliza mwaka 2009 na sisi tulifanya mtihani wa kidato cha pili na alifeli mmoja wengine tukasonga mbele. Tujitahidi kuwa na data ili kufikisha ujumbe ulio sahihi mkuu. NI HAYO TU.