Waliomburuza na gari mama muuza ndimu wasimamishwa kazi Kenya

Shadow7

JF-Expert Member
Joined
Sep 28, 2020
Posts
24,606
Reaction score
39,289
Gavana wa kaunti ya Kisumu amewasimamisha kazi maafisa waliomburuza barabarani mwanamke mfanyabiashara wa matunda.

ddd.jpeg

Vyombo vya habari vimeripoti kuwa mwanamke huyo alikataa kutoa rushwa. Alikuwa akiuza machungwa na ndimu njia ya wapita kwa miguu eneo ambalo limepigwa marufuku kufanyika biashara.

pqftovw0mf7x3t605c189147aca.jpeg

Mwanamke huyo aliwaambia waandishi wa habari kuwa mmoja kati ya maafisa hao alikaa kwenye gari aina ya pick-up akiwa amemshika mkono wake na kukataa kumuachilia wakati gari hiyo ilipokuwa ikiondoka.

download-9.jpeg

Dereva aliendesha chombo hicho cha moto mpaka katika kituo cha polisi cha karibu baada ya kundi la watu kuamua kukimbiza gari. Polisi walifyatua mabomu ya kutoa machozi kuwatawanya watu waliokuwa na ghadhabu waliokusanyika katika kituo hicho.

Gavana Anyang’Nyong’o amesema amewasimamisha kazi maafisa wote waliohusika na tukio hilo mpaka uchunguzi utakapokamilika.
 
Daaah bora Nyerere alitunyonyesha ujamaa na tukaja kukulia kwenye ubepari
 
KENYA
nchi ambayo m tu anakula mtu

Na Kuna wapumbavu wanasema bongo bahati mbaya
 
wahuni wamevalia sare za polisi. hivi kwa nini mbona wanamtesa mama? natumai hatua kali zitachukuliwa dhidi yao
 
hii sio kweli. hawa ni wahuni wawili/ watatu tu waliokosa akili
Wakenya ni watu makatili,wabinafsi na wenye roho mbaya sana
Angalia akili za Ruto kakaa nyumbani kwake kaamua kupiga marufuku mahindi ya Tanzania eti yana sumu kuvu,halafu anaingiza ya toka shambani kwake DRC
 
Mambo kama haya huwa yananiuma sana sana, nahisi kwakua nilinyanyaswa sana utotoni. I'm man but can't stop wiping tears. This is shit!
 
Wakenya ni watu makatili,wabinafsi na wenye roho mbaya sana
Angalia akili za Ruto kakaa nyumbani kwake kaamua kupiga marufuku mahindi ya Tanzania eti yana sumu kuvu,halafu anaingiza ya toka shambani kwake DRC
kumbe hasira zote hizi ni kwa sababu ulikosa soko la mahindi Kenya? haha!
yupo jamaa mmoja alimiminiwa risasi 36 kwa mwili wake ndani ya Tanzania, je itakua sahihi nikisema kwamba Watanzania ni wakatili, washamba na wenye roho ngumu/ nyeusi?
 
kumbe hasira zote hizi ni kwa sababu ulikosa soko la mahindi Kenya? haha!
yupo jamaa mmoja alimiminiwa risasi 36 kwa mwili wake ndani ya Tanzania, je itakua sahihi nikisema kwamba Watanzani ni wakatili, washamba na wenye roho ngumu/ nyeusi?
Na yule aliekatwa kiganja Kisha akang"olewa koromero?
Vipi yule makaburi aliemiminiwa risasi 300 mbele ya wajukuu zake,usisahau Askari Mombasa walicharaza viboko kina mama mpaka kuwachania chupi kisa wanatekeleza lock down
 
unajua kilichomsibu Akwilina??? je yu wapi Azory Gwanda? Ben Saanane?
vipi wale vifaranga 3,000 vya mfanyabiashara kuteketezwa hadi kugeuka jivu? unakumbuka wale ng'ombe 4,000 wa watu jameni walivyotaifishwa bila huruma?
 
Wakenya ni watu makatili,wabinafsi na wenye roho mbaya sana
Angalia akili za Ruto kakaa nyumbani kwake kaamua kupiga marufuku mahindi ya Tanzania eti yana sumu kuvu,halafu anaingiza ya toka shambani kwake DRC

Hawa ilipaswa wafungwe gerezani hata sio kusimamishwa kazi tu, mgambo huwa na tabia za hovyoo kote, nimeshuhudia ukatili wao Tanzania pia acheni kujifanya watakatifu, kwanza nyie ukatili wenu umefichwa kabisa maana media zenu haziruhusiwi kuandka chochote ila misifa tu. Miili inaopolew kwa mifuko ya sandarusi kwenu huko na nchi yote kimyaaa!!!!

Gavana wa kaunti ya Kisumu amewasimamisha kazi maafisa waliomburuza barabarani mwanamke mfanyabiashara wa matunda.

ddd.jpeg

Vyombo vya habari vimeripoti kuwa mwanamke huyo alikataa kutoa rushwa. Alikuwa akiuza machungwa na ndimu njia ya wapita kwa miguu eneo ambalo limepigwa marufuku kufanyika biashara.

pqftovw0mf7x3t605c189147aca.jpeg

Mwanamke huyo aliwaambia waandishi wa habari kuwa mmoja kati ya maafisa hao alikaa kwenye gari aina ya pick-up akiwa amemshika mkono wake na kukataa kumuachilia wakati gari hiyo ilipokuwa ikiondoka.

download-9.jpeg

Dereva aliendesha chombo hicho cha moto mpaka katika kituo cha polisi cha karibu baada ya kundi la watu kuamua kukimbiza gari. Polisi walifyatua mabomu ya kutoa machozi kuwatawanya watu waliokuwa na ghadhabu waliokusanyika katika kituo hicho.

Gavana Anyang’Nyong’o amesema amewasimamisha kazi maafisa wote waliohusika na tukio hilo mpaka uchunguzi utakapokamilika.
Adui namba moja wa mtu mweusi, ni mtu mweusi mwenziye. Wazungu wanatushaa kwa matendo yetu ya ajabu na kutufananisha na 🦍🦍🦍🙈🙉🙊🐵🐒 ya Kigogo wa Twitter
 
Back
Top Bottom