Mkalukungone Mwamba
JF-Expert Member
- Aug 29, 2022
- 3,141
- 7,205
Watu wawili wanaodaiwa kuhusika na mauaji ya kijana mmoja, jinsi ya kiume ambaye awali hakutambuliwa huku kiwiliwili chake kikiwa kimetenganishwa na kichwa chake kwa kukatwa na kitu chenye ncha kali (panga) na kupelekwa kusikojulikana, wameuawa baada ya kushambuliwa na wananchi wenye hasira kali walipokuwa wakionesha mali na kichwa cha marehemu kilipofichwa.
Itakumbukwa tukio hilo lilitokea Agosti 8, 2025 katika Mtaa wa Malimbe, Kata ya Luchelele Jijini Mwanza kando ya Barabara ya Luchelele ambapo mwili wa kijana huyo aliyetambuliwa kwa jina la Dickson Madaraka Yusuph (24)- dereva bodaboda na Mkazi wa Mtaa wa Shadi Kata ya Luchelele ulikutwa huku kichwa kikiwa hakipo.
Akitoa taarifa hiyo kwa waandishi wa habari siku ya Jumatatu, Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, SACP Gideon Msuya amewataja waliouawa kuwa ni Oscar Emmanuel (20) na Edwin Bujuel (22) wakazi wa Mtaa wa Shadi, Kata ya Luchelele ambapo amedai baada ya kukamatwa walikiri kuhusika na tukio hilo huku chanzo kikiwa ni wivu wa kimapenzi.