Waliomponda Magufuli ndio hao hao wanaolamika umeme kukatika

Afadhali tukae kwenye giza rather than living with a KILLER
 
Shida ya umeme ilianza 1991,na haijawahi tatuliwa ikaisha kabisa,wakati wa magu umeme ulikua ukikatika pia,shida ya umeme tz hapa kati haikutokana na kiwango Cha umeme unaozalishwa Bali miundombinu kumpelekea mlaji,labda jnhp likikamilika shida itapungua
 
Jinga kabisa!!!! Kwa hiyo hatuna mvua za kutosha sasa!!!??
 
Kuna kitu kimekupiga chenga ya mwili. Kipindi cha Adolf Hitler, Ujerumani ilifikia kiwango cha juu sana cha maendeleo. Treni zilikuwa zikizingatia muda wa safari hadi kwa nukta zilizopangwa. Bidhaa na huduma zote zilikuwa zikipatikana kwa viwango na ufanisi wa hali ya juu sana. Ujerumani iliongoza kwa teknolojia na uchumi wa viwanda Ulaya nzima. “Made in Germany” haikuwa na mpinzani.

LAKINI, pamoja na yote hayo, Hitler na wenzake wa (NAZI Party) wanatambulika kwa mauaji ya kimbari yanayofahamika kama holocaust. Hadi leo wanaitwa “wanaharamu” (bastards). Habari ya “mazuri” ya Hitler haipo na haiyumkiniki.

Kuna mambo mabaya ukiwatendea binadamu wenzako kwa kudhamiria hapa duniani yanafunika mengine yote! Mizani ya mabaya na mazuri haifanyi kazi hapo. Dawa ni kutubu na kuwaomba msamaha wote uliowadhuru kabla ya mwisho wako. Hitler alijiua kuliko “fedheha”.
 
Kipindi hiki mvua hakuna?
 
Watakuambia uongozi wa saa100 ni mzuri zaid kuliko jpm kwa kuwa tu wameruhusiwa kuiba bila ya kuulizwa na kutunisha matumbo yao ..hawanaga hoja ya maana
Hakuna awamu ya URais hapa Tanzania ambapo ufisadi na mafisadi hawakuwepo.

Btw hakuna ufisadi unaoweza kufanikiwa bila Ikulu kuhusika. Tunazungumzia mabilioni kwenye miradi, manunuzi na toka BOT moja kwa moja - sio vimilioni, vilaki na vibuku vya kupigia kiwi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…