Waliomteka Tarimo (akina Benki) wamerudi uraiani dhamana yao imepita kimyakimya, kesi kuendelea Januari 9, 2025

Waliomteka Tarimo (akina Benki) wamerudi uraiani dhamana yao imepita kimyakimya, kesi kuendelea Januari 9, 2025

Wakuu,

Kama mnavyojua watuhumiwa wa tukio la utekaji wa Talimo kule Kilivya, Benki na wenzake 5 walikamatwa Disemba 4 na kufikishwa mahakamani Disemba 6.

Ikumbukwe kuwa dhamana yao ilikuwa wazi kwa masharati ya kulipa Bondi ya Shilingi Milioni 10 na wadhamini wawili kwa Kila mmoja, pamoja na kutosafiri nje ya Dar es Salaam bila kibali cha mahakama.

Sasa bwana jamaa wamepata dhamana kimyakimya na sasa wapo uraiani wakifuatilia mwenendo wa kesi, Benki alionekana sehemu yake ya kazi jana na leo kwenye kituo cha Magufuli alipokuwa kama mlinzi shirikishi.

Pia soma: Watuhumiwa waliotaka kumteka Deogratius Tarimo (Deo Bonge) wafikishwa Mahakamani

Hivi kwa kesi kama ya akina Benki mtu anaruhusiwa kurudi kazini kuendelea na majukumu yake kama kawaida au anasimamishwa hadi atakapokuwa cleared na charges? Wanasheria Pascal Mayalla tunaomba ufafanuzi hapa.

Kwanini dhamana hii imepita kimyakimya though na vile wanancgi tulivyokuwa invested kufatilia mwenendo wa kesi hii?

Wanataka tusahau waachiliwe warudi uraiani kuteka watu wengine kwenye list?

=====

Muhtasari wa kilichokea Dec 19, 2024 Makamani

Mahakama ya Hakimu Mkazi ilishindwa kusikiliza kesi ya Jaribio la Utekaji inayowakabili Watu Sita dhidi ya Mfanyabiashara Deogratius Tarimo baada ya upande wa Mashtaka kusema hoja za awali bado hazijawa tayari.

Watuhumiwa walitakiwa kusomewa maelezo ya awali mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu Ramadhani Rugemalila, Wakili wa Jamhuri, Makalala akaiambia Mahakama kuwa shauri hilo liahirishwe kwa kuwa hoja hazijawa tayari.

Mahakama iliahirisha shauri hilo hadi Januari 9, 2025 itakapotajwa tena huku watuhumiwa wakipewa fursa ya dhamana endapo watatimiza masharti.
Kitendo walichotaka kutekeleza ni kitendo cha kigaidi hivyo hawakustahili kabisa kupata dhamana. Hii kesi ni geresha tu hawa ni timu Mafwele
 
Chagua Moja: Fanya kazi na wasiojulikana, gharama kubwa ila hakuta kuwa na kesi; Fanya kazi na majambazi ya mtaa, gharama ndogo, ila kuna chance kubwa ya kudakwa.
 
Dawa ni kwamba wakisharejea mtaani wanapaswa kushughulikiwa na raia kisawa sawa huko kwenye sheria ni uozo mtupu
 
Back
Top Bottom