yeye huyo mkeo mshahara wake unatumika kwenye nini? mimi ni mwanamke lakini siwez kufanya hio dhambi ningejitegemea nauli na mambo yangu personal ibakie kama ntakwama siku moja moja anisaidie baba chanja lakini sio hivo.
Si bora hiyo kuna mmoja na mfahamu, kaachiwa gesti moja, bar,fremu za biashara kama nne,nyumba mbili zina wapangaji full, kafunguliwa frem ya duka la nguo, mtaji kapewa na mmewe. Ila bado anahitaji hela ya matumizi,kila mwezi,anahitaji hela ya kulipiwa kodi ya fremu yake ya biashara na hela ya mafuta ya gari anayo tembelea na matumizi mengine binafsi na mtaji ukikatika mmewe anatoa.
Hela ya gesti, nyumba mbili zenye wapangaji, fremu tatu za biashara na biashara zake binafsi hata yy mwenyewe hajui kazipeleka wapi,mmewe kuna kipindi alipataga changamoto za kiuchumi ila mkewe hakumsupport.
Kuna mwan mmoja dereva wa bajaj, sasa kuna usiku mmoja alikesha ila biashara haikuwa nzuri. Asubuhi mkewe anataka hela ya pampas, akamwambia kama ana kaakiba akanunue,ila mchana akiingia mzigoni atampa,demu kakomaa ila jamaa akambembeleza ,baadae akamfunga mtoto vikanga. Sasa mwana siku hiyo alichelewa kuamka halafu simu, alijitupia alivyo rudi usiku wa jana,mke kaenda kununua vitafunio. Mwamba tafuta sana simu yake wapi,vurugua kitanda,kwenye makochi,upande wake kabatini ila wapi. Akasema ngoja angalie upande wa mkewe,kupekua pekua anakutana 1.2m,anamuuliza mkewe kwa aibu anadai mzee wao aliuza kiwanja alimpa kila mtu 1.5m kwa hiyo yy kishatumia 300k kabakiwa na hiyo 1.2m,mwana alichoka, yaani mkewe kitoa mia tano kwenye 1.2m ya pampas alishindwa. Sometimes si wa nyumbani wala wanao fanya kazi ,kiasili mwanamke ni mbinafsi japo wachache sana wanaokubali kushare. Haya mambo sometimes yaani kuomba Mungu, halafu wanavyo wasumbua wachungaji na waganga wakienyeji kwenye kutafuta waume, wakiwapata wanawatenda hivi.
Ndio maana kuna wazee wanasema kwenye nyumba kama mke ana milioni,mume ana laki mbili basi jumla nyumba ina milioni mbili.