PreGE2025 Walioondoka CHADEMA, UWT Njombe yawakaribisha CCM yasema wasije na vurugu

PreGE2025 Walioondoka CHADEMA, UWT Njombe yawakaribisha CCM yasema wasije na vurugu

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

The Watchman

JF-Expert Member
Joined
Nov 7, 2023
Posts
2,186
Reaction score
4,940
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Umoja wa Wanawake (UWT) mkoa wa Njombe Dkt. Scholastika Kevela amewataka viongozi na wanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) mkoa wa Njombe waliojiondoa na Chama hicho kujiunga na CCM akidai kuwa Chama chao kina utaratibu wa kusikilizana.

Dkt. Scholastika Kevela ameeleza hayo mjini Njombe wakati akizungumza na wajumbe wa baraza la UWT wilaya ya Njombe ambapo kamati ya Utekelezaji UWT mkoa wa Njombe imekutana na viongozi hao kwa lengo la kujadili mambo mbalimbali ya kuimarisha Chama na Jumuiya.

Kupata matukio na taarifa zote kwa kila mkoa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025 ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

"Nimeskia (CHADEMA) Njombe pia wanagawana vilago,sisi tunawakaribisha milango iko wazi ila wasije na vurugu,Chama cha Mapinduzi tunasikilizana kwa hiyo yakiwashinda huko njoeni"amesema Dkt.Scholastika

Dkt. Scholastika ameyezungumza hayo ikiwa tayari viongozi mbalimbali wandamizi wa CHADEMA Njombe akiwemo Veronica Mlonganile Mwenyekiti wa Baraza la wanawake Chadema (BAWACHA) mkoa, Patrick Njulumi Mwenyekiti wa CHADEMA wilaya ya Wanging'ombe, Leah Masasi Mwenyekiti wa Baraza la wanawake Jimbo la Lupembe pamoja na wanachama wengine ishirini wa CHADEMA wakitangaza kujivua uanachama.

 
Back
Top Bottom