Waliopewa chanjo ya kwanza ya Corona waonyesha matumaini kwa kupata kingamwili

Waliopewa chanjo ya kwanza ya Corona waonyesha matumaini kwa kupata kingamwili

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,618
Reaction score
9,611
Mkutano wa kuthibitisha matokeo ya majaribio ya Chanjo ya kwanza ya virusi vya Corona iliyotengenezwa na Taasisi ya bidhaa za viumbe ya Wuhan ya China umefanyika jana kwa wakati mmoja mjini Beijing na mkoani Henan.

Matokeo yameonesha kuwa baada ya kupewa chanjo aina hiyo, hakuna mtu aliyekuwa na dalili mbaya, na wote wamepata kingamwili dhidi ya virusi vya Corona.

Majaribio hayo yalifanyika kwa siku 66 chini ya uongozi wa Kituo cha kinga na udhibiti wa magonjwa cha mkoa wa Henan, na kuonesha matokeo kamili ikiwemo data kuhusu usalama na ufanisi wa chanjo, pamoja na matokeo ya utafiti kuhusu watu wenye umri tofauti ambao walipewa chanjo kwa kiasi tofauti na kwa utaratibu tofauti.

Swahili.cri
 
Acheni story
Semeni tuelewe kinga au chanjo imepatikana au bado?
Sio story sijui watu 66 oooh umri tofauti kuweni wazi
 
Wanahangaika tu waswahili tudhajitengenezea kinga wenyewe na corona kaamua kikimbia
 
Acheni story
Semeni tuelewe kinga au chanjo imepatikana au bado?
Sio story sijui watu 66 oooh umri tofauti kuweni wazi
😂😂
Haya sasa wabongo na chanjo ya Wuhan wanataka uwazi..😅
 
Bado wanateseka na kinga dah si bora waje kuchukua nyungu za bongo, tangawizi na limao ni kinga tosha
 
Back
Top Bottom