Waliopewa jukumu la uongozi ngazi za chini wanadidimiza nchi

Waliopewa jukumu la uongozi ngazi za chini wanadidimiza nchi

Trainee

JF-Expert Member
Joined
Sep 22, 2018
Posts
2,660
Reaction score
3,501
Aisee serikali inabidi iangalie sana kwenye baadhi ya mambo laa sivyo waliopewa jukumu la uongozi ngazi za chini hizi wanadidimiza nchi

1. Mtendaji kata nyumba ya serikali anaipangisha anakuwa anapata hela ya mboga

2. Mtendaji kata ameuza maeneo ya serikali (maeneo kuzunguka ofisi ya kata) halafu yeye amestaafu zake

3. Ujenzi wa madarasa haya mapya diwani anamuamuru2 fundi ampe laki tatu kwani bila yeye asingepata kazi

4. Asilimia 20 ya nguvu za jamii kwenye mradi wa ujenzi shuleni msingi kijiji hakijachangia hata mia. Tatizo diwani mwenyekiti wa kijiji na mtendaji wa kijiji- sababu eti hela hakuna bado wapo kwenye mchakato

5. Kuna fungu la kijiji kwenda katani mkuu wa wilaya alisitisha kusipelekwe tena cha ajabu mtendaji kata na diwani wake wameamrisha fungu hilo lipelekwe eti wanaielekeza kwenye kuchimba shimo choo Sekondari (rejea namba 4)

6. Ukirejea namba 4 (ambapo kuna deni kama la milioni 3 kwenye mradi), bado hakujafanyiwa lolote shuleni ila eti kuna mihtasari/bajeti inaandaliwa kwajili ya kujenga kituo cha utayari (fedha iliyopo inayopigiwa hesabu zote hizo ni milioni 4)

7. Miti inakatwa Hifadhi za misitu zinateketea kwa kasi lakini hakuna kinachofanyika kudhibiti mbaya zaidi ukiuliza unaoneshwa kibali kuruhusu uchafuzi huo kutoka kijijini/katani (mbAya zaidi vijiji vina kamatti za misitu tu hakuna wataalamu wa misitu kwahiyo wao wanachoangalia ni kupiga pesa tu ila elimu ya mazingira/misitu ni sifuri)

8. Migodi holela uvunaji wa misitu kiholela na kila kazi zinazofanyika illegal unakuta viongozi wa kata /kijiji wana share zao

9. Drop out ya watoto shuleni inapanda kila siku na kila siku ofisi zinakabidhiwa orodha lakini hakuna kinachofanyika

10. Kuna mambo mengi mengine ambayo siwezi kuyaandika hapa yote ila itoshe tu kwa hayo.

Yaani hizi nafasi tatu ni majipu na serikali isipokuwa makini hizo nafasi zinaharibu nchi/taifa:

DIWANI
MTENDAJI KATA/KIJIJ
MWENYEKITI WA KIJIJI

Sababu kubwa niliyoona ni moja tu nayo ni WAZAWA. Yaani top authorities zote zinashikiliwa na wazawa kwahiyo wanaendesha mambo kwa mazoea na kujuana tu.
 
We Machinga! Tafuta pesa wewe achana na umbea
 
Back
Top Bottom