Analogia Malenga
JF-Expert Member
- Feb 24, 2012
- 5,108
- 10,191
Pasi maalumu ya Umoja wa Ulaya, itakayoanza kutumika tarehe 1 mwezi Julai kurahisisha safari kwenda Ulaya kwa wale waliopata chanjo itaanza kufanya kazi lakini ikiwa na sharti moja muhimu.
Mtu yeyote aliyepewa chanjo ya AstraZeneca inayozalishwa na Taasisi ya Serum ya India hatastahiki kupata pasi hiyo- na hiyo inajumuisha raia wengi wa nchi za kipato cha chini na cha kati ambao walipatiwa chanjo zilizosambazwa na mpango wa COVAX uliofadhiliwa na WHO.
Hii ni kwasababu pasi maalumu ya Umoja wa Ulaya itatambua tu toleo la Vaxzevria la chanjo ya AstraZeneca ambayo ilitengenezwa nchini Uingereza au maeneo mengine ya Ulaya, na hivyo kupitishwa na Wakala wa Dawa wa Ulaya (EMA). Kwa upande mwingine, ununuzi na usambazaji mkubwa wa chanjo chini ya mpango wa COVAX unahusisha chanjo ya AstraZeneca, iliyotengenezwa na Taasisi ya Serum ya India.
Wakati hayo yakijiri, Rais wa Uganda Yoweri Museveni ametahadharisha uwepo "ubinafsi wa chanjo" ulimwenguni lakini akasema "itawaamsha" Waafrika kujitosheleza.
Rais Museveni amesema kuwa Afrika wanahitaji malighafi kuzalisha chanjo zao wenyewe na sio michango ya chanjo kutoka nchi zilizoendelea.
‘’Ni aibu kwetu sisi Waafrika. Kwanini tutegemee kila kitu kutoka nje. Hii ni aibu kwa Afrika, ‘’ aliwaambia wajumbe waliohudhuria mkutano wa Shirika la Afya duniani, Jumapili.
Rais Museveni alisema kuwa nchi za bara la Afrika zinapaswa kuacha kusubiri chanjo za misaada na kutengeneza zao wenyewe.
‘’Ubinafsi duniani ni mbaya, lakini ni vizuri. Ninaupenda kwa kuwa unawaamsha Waafrika. Ni aibu kwa bara zima la Afrika limelala, likisubiri kuokolewa na wengine kama ilivyotokea wakatu wa biashara ya utumwa,’’ alisema.
Rais Museveni amesema Uganda ilikuwa kwenye mchakato wa kutengeneza Chanjo yake yenyewe na ilikuwa inahitaji tu msaada wa malighafi akisema,‘’Msiwe na shaka tutanunua. Hatuhitaji msaada.’’