Waliopoteza maisha katika ajali ya ndege iliyotokea Florida, watambuliwa

Waliopoteza maisha katika ajali ya ndege iliyotokea Florida, watambuliwa

Atukuzwaye

Senior Member
Joined
Oct 5, 2026
Posts
191
Reaction score
250
Watu tisa wamefariki dunia baada ya ndege ndogo ya kifahari (private jet) kuanguka na kulipuka nchini Marekani, jimbo la Florida, siku ya Jumapili.

Miongoni mwa waliofariki ni mfanyabiashara wa teknolojia Adam Robinson, mke wake Helen Sharp pamoja na watoto wao wawili, kwa mujibu wa taarifa ya pamoja iliyotolewa na baadhi ya familia za marehemu.
Wengine waliokuwa ndani ya ndege hiyo ni Rachel Reed, Charmi Fehr na Anita Maria Cetina, ambao pia walikuwa wakisafiri pamoja na familia ya Robinson.

Kwa mujibu wa kampuni ya East Coast Jets, rubani wa ndege hiyo aliyetambuliwa ni Jeff Gregory (55), huku rubani msaidizi Nathalia Filgueiras (20) naye akipoteza maisha katika ajali hiyo.

Soma pia: Ajali ya ndege imetokea jimbo la Florida na kusababisha vifo vya watu 9


Nine people have been killed after a small jet crashed and exploded in Florida on Sunday.  Among.jpg

Nine people have been killed after a small jet crashed and exploded in Florida on Sunday.  Amo...jpg
Nine people have been killed after a small jet crashed and exploded in Florida on Sunday.  Amo...jpg
Nine people have been killed after a small jet crashed and exploded in Florida on Sunday.  Amo...jpg
 
usafiri salama zaidi lakini likitokea la kutokea.. uwezekano wa kupona ni 0.000001.
 
Back
Top Bottom