Waliosaidia Assad apinduliwe ni Russia ama Marekani?

Waliosaidia Assad apinduliwe ni Russia ama Marekani?

Kuna watu huwa wanawaona waarabu kama hawana akili za kujitegemea.

Sasa Bashir Assad kaondolewa madarakani. Jee kaondolewa na Wasiria peke yao ama hao Wasiria wamesaidiwa na Marekani au Russia?

Kama Russia kwa maslahi gani na kama pia na Marekani, pia ni Kwa maslahi gani?
Kwanza ni Uturuki, pili ni mataifa ya kiarabu yaliyo Sunni kwani Iran inayomsaidia Syria ni Shia na pia wamechoshwa na makundi ya kigaidi hasa Herzebolah ambayo msaada mkubwa wa silaha kwenda kwa.magaidi ulikuwa ukipitia Syria kutoka Iran, inasadikika USA alizuia jeshi kutoka iraq lililokuwa linakuja kumsaidia Asadi na ni wakati mzuri kwa Israel sababu Herzebolah watakosa nguvu.
 
Nani alikuwa nguvu nyuma ya nguvu zake?

Maana nilidhani ni watu wa Uarabiuni.
 
Kuna watu huwa wanawaona waarabu kama hawana akili za kujitegemea.
Siyo Waarabu tu, ni pamja na Masuria wao weusi
Sasa Bashir Assad kaondolewa madarakani. Jee kaondolewa na Wasiria peke yao ama hao Wasiria wamesaidiwa na Marekani au Russia?

Kama Russia kwa maslahi gani na kama pia na Marekani, pia ni Kwa maslahi gani?
Wale Masuria wa Waarabu wanasema Russia ndiyo kamwambia akabidhi nchi.

Waasi wanasema wamempindua Assad, dunia imeona Assad akipinduliwa na kukimbilia Russia.

Russia alitaka kuingilia akashindwa apite vipi kufika Syria wakati Turkey alipomgomea na kumwambia akithubutu kupitisha ndege kwenye anga lake ataitungua na Russia anakumbuka Turkey aliwahi kuitungua kweli ndege yake.

Russia hakuwa na namna, akanywea na kumuambia Assad kimbia njoo Moscow.

Waka activate makundi yao yaliyokuwa Iraq, yalipoanza kuelekea Syria tu, UK, US na Israel wakawatekeza wote.

Houth nao wakawa wameshakuwa crippled, wameki wanatweta, msemaji wao anaoneana kwenye Telegram Channel tu.
 
Back
Top Bottom