Uchaguzi 2020 Walioshindwa CCM ni lulu kwa vyama vya upinzani

Bwana wako Bashite anatakiwa na nani? Yule hata ujumbe wa nyumba kumi hawezi kupata.
 
Nawashangaa ACT kuendelea kuwa kapu la mabaki ya lumumba
Mamluki hawana nafasi tena, upinzani ni chuo cha siasa kinajitosheleza kuwapika vijana wapo underground upcoming wengi Sana kuliko nafasi zote za uongozi zilizopo
 
Umeonaeeeee? Eti Bashite atakiwe na chama gani? Labda kwenye tawi la ccm ACT na NCCR n CUF ya Lipumba
Bashite hawezi kuwa mbunge najua hasira zimekujaa @Wakudadavua
 
Sasa kina lijualikali na Silinde wapo wanauguza vidonda
Mkuu unadhani mwaka huu kuna watu watatimkia huko? Mmewapa somo la kutosha, wale walio unga juhudi wamenyolewa vipara bila kutiwa maji!!
 
Samahani kidogo mh. Naibu; swali nje ya mada! Kura zako zilitohaaaaa?! Au unagombania vile viti ‘dhaifu’!
 
Akili nyembamba kama tissue utazitambua tu.Ukakaa,ukawashwa ndiyo ukaja na utopolo huu?Hasara mbinguni na duniani.😂😂😂
 
Jidanganye, CHADEMA mbona walishamaliza kura za maoni! Wacha wakae bench! Mtu kama Mlinga naye unamwita jembe huyo?
 
Huyo Milinga wenyewe wana lumumba wanamuona ni jembe hasa kwa kutukana matusi viongozi wa upinzani.
Jidanganye, CHADEMA mbona walishamaliza kura za maoni! Wacha wakae bench! Mtu kama Mlinga naye unamwita jembe huyo?
 
Kuchujwa kwenye kugombea uongozi kwenye chama kimoja, ukakimbilia chama kingine, ni dalili fika ya uchu wa madaraka. Hivyo ndivyo alivyofanya Lowassa mwaka 2015. Watia nia wakiwa wengi na chama kikapendekeza mmoja wao, wale ambao hawakupendekezwa shurti wakubali uamuzi huo na kumuunga mkono aliyependekezwa. Hiyo ndiyo demokrasia. Kuthubutu kwako kujitokeza kuomba usimamishwe kugombea ni haki yako. Lakini kuchaguliwa mmoja kati ya waliojitokeza, ndiyo mwisho wa kutia nia kwako wewe uliyeachwa. Ulijiona unafaa. Chama kikakuona kweli unafaa lakini mwingine anafaa zaidi. Ndiyo kisa cha kumchagua huyo. Kama wote waliotia nia wakikomaa wasimamishwe wenyewe tu si itakuwa balaa?

Mfano mzuri ulionyeshwa na Rais Magufuli aliposhindwa mara tatu katika uchaguzi wa ubunge. Mara zote alikuwa akiyakubali matokeo kwamba "The people have spoken". Wapiga kura walikuwa hawajui ni nani wanayemkataa. Hata Biblia inasema jiwe alilolikataa fundi mwashi ndiyo limekuwa msingi wa nyumba. Sura nyingine ya Biblia inasema wasamehe kwa kuwa hawajui watendalo. Baada ya takriban miaka hii mitano ya urais wa Magufuli, bila shaka wapiga kura wa Biharamulo wametambua walikuwa hawajui nani waliyekuwa wakimkataa.

Wosia wangu kwa mpiga kura ni kwamba chagua mtu atakayekuletea maendeleo. Siyo kuchagua mtu mwenye uchu tu wa madaraka. Kipofu tu ndiye haoni uwezo wa Magufuli katika kuiendeleza Tanzania. Upinzani unachong'ang'ania ni kumuondoa tu Rais Magufuli madarakani, bila kusema ni kitu gani bora zaidi wao watakufanyia wewe mpiga kura. Ni uchu wa madaraka tu. Mpiga kura kumbuka msemo kwamba zimwi likujualo halikuli likakwisha. Lissu anatajwa sana na upinzani asimame kushindana na Magufuli ambaye tayari ameonyesha nini anaweza kuifanyia Tanzania. Mfano mmoja ni sheria ya madini ambayo Rais Magufuli amebadilisha kwa manufaa ya Tanzania, hata kama bado mpaka sasa hatujalipwa kiasi chote kilichokuwa kikiibiwa. Lissu alikuwa akikomaa Bungeni kwamba tukiwagusa hao mabeberu tutapelekwa mahakamani kwa kuwa tulitia sahihi mkataba. Lissu huyo huyo aling'ang'ana pia Bungeni kuwa kunana mkataba sijui wa lini ambao unasema ziwa Nyasa lote ni la Malawi. Vivyo hivyo alitaja mkataba uliosainiwa kati ya Uingereza na Misri ukitukataza Tanzania kuchukua maji kutoka Ziwa Victoria kupeleka Tabora na Dodoma. Wewe mpiga kura wa Tanzania jiulize mtu kama huyu akiwa Rais si atakuwa anapigania manufaa ya nchi nyingine tu?.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…