Walioshindwa Kurejesha Mawasiliano Somanga Kuchukuliwa Hatua: Ulega

Walioshindwa Kurejesha Mawasiliano Somanga Kuchukuliwa Hatua: Ulega

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2020
Posts
3,119
Reaction score
1,430

WALIOSHINDWA KUREJESHA MAWASILIANO SOMANGA KUCHUKULIWA HATUA: ULEGA​

Waziri wa Ujenzi, Abdallah Ulega amesisitiza kuwachukulia hatua kali za kinidhamu wataalam kutoka Wakala wa Barabara (TANROADS) waliouhusika na uzembe wa kushindwa kurejesha kwa wakati mawasiliano ya barabara kuu ya Dar es Salaam - Lindi eneo la Somanga Mtama Mkoani Lindi

Ulega ameeleza hayo Mkoani Lindi wakati alipofika na kukagua kazi za urejeshaji wa mawasiliano hayo yaliyokatika tarehe 06 Aprili, 2025 na kutoridhishwa na kasi ya urejeshaji wa mawasiliano hayo na kuelekeza wataalam kutoka kwa TANROADS kutoondoka eneo hilo hadi mawasiliano hayo yatakaporejea.

“Nimekagua na nimeona namna kazi inavyoendelea, mimi kama Kiongozi nimeona kuna jambo ambalo bado halijafanyika kisawasawa, uko uzembe uliofanyika, nitachukua hatua kali ili siku zingine yatakapotea mambo ya dharura kama haya yachukuliwe kidharura”, amesema Ulega.

Ulega ametoa salamu za pole kwa wananchi wa Mikoa ya Kusini na Dar es Salaam waliokumbwa na kadhia hiyo na kuwahakikishia kuwa timu ya wataalam iliyopo itafanya kazi haraka iwezekanavyo ili kuruhusu wananchi waliokwama kuendelea na safari zao.

Halidhalika, ameipongeza timu ya wataalam ya TANROADS Mkoa wa Lindi kwa kuchukua jitihada za dharura mara baada ya tukio hilo kutokea na kusisitiza kuongezwa kwa idadi ya malori ya mawe hadi kufika magari 100 ili yasaidie kwa haraka urejeshaji wa barabara katika eneo hilo.

Akizungumza na wananchi wa Somanga, Ulega ameeleza kuwa Mhe Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ameidhinisha zaidi ya Shilingi Bilioni 130 kwa ajili ya ujenzi wa madaraja yaliyokatika katika Mkoa wa Lindi na kubainisha kuwa hatua za ujenzi wa madaraja matano zinaendelea na yapo katika hatua mbalimbali za utekelezaji.

Ameongeza kuwa Serikali inatambua umuhimu wa barabara hiyo na katika mwaka mpya wa fedha 2025/2026 itakarabati na kuziba mashimo katika maeneo korofi ya Marendego, Somanga, Njia Nne, Matandu, Ikwriri - Nyamwage - Chumbi ili kurahisisha huduma za usafiri wa abiria na mizigo.

Vilevile, Serikali itaanza utekelezaji wa ujenzi wa barabara kwa njia nne kuanzia Kongowe - Mbagala Rangi tatu ambapo tayari Mkandarasi ameshapatikana na pia ujenzi wa barabara kuanzia Kongowe hadi Mkuranga itajengwa kwa njia nne ili kupunguza msongamano wa magari uliopo sasa.
 

Attachments

  • WALIOSHINDWA KUREJESHA MAWASILIANO YA BARABARA SOMANGA - MTAMA KUCHUKULIWA HATUA.MP4
    45.8 MB
  • WhatsApp Image 2025-04-07 at 19.33.59.jpeg
    WhatsApp Image 2025-04-07 at 19.33.59.jpeg
    464.7 KB · Views: 36
  • WhatsApp Image 2025-04-07 at 19.33.59 (1).jpeg
    WhatsApp Image 2025-04-07 at 19.33.59 (1).jpeg
    519.9 KB · Views: 36
  • WhatsApp Image 2025-04-07 at 19.34.00.jpeg
    WhatsApp Image 2025-04-07 at 19.34.00.jpeg
    575.6 KB · Views: 43
  • WhatsApp Image 2025-04-07 at 19.34.01.jpeg
    WhatsApp Image 2025-04-07 at 19.34.01.jpeg
    894.3 KB · Views: 48
  • WhatsApp Image 2025-04-07 at 19.34.02.jpeg
    WhatsApp Image 2025-04-07 at 19.34.02.jpeg
    567.2 KB · Views: 47
  • WhatsApp Image 2025-04-07 at 19.34.02 (1).jpeg
    WhatsApp Image 2025-04-07 at 19.34.02 (1).jpeg
    301.9 KB · Views: 40
  • WhatsApp Image 2025-04-07 at 19.34.03.jpeg
    WhatsApp Image 2025-04-07 at 19.34.03.jpeg
    286.8 KB · Views: 45
  • WhatsApp Image 2025-04-07 at 19.34.03 (1).jpeg
    WhatsApp Image 2025-04-07 at 19.34.03 (1).jpeg
    205.3 KB · Views: 48
  • WhatsApp Image 2025-04-07 at 19.34.04.jpeg
    WhatsApp Image 2025-04-07 at 19.34.04.jpeg
    304.8 KB · Views: 42
  • WhatsApp Image 2025-04-07 at 19.34.05.jpeg
    WhatsApp Image 2025-04-07 at 19.34.05.jpeg
    534.6 KB · Views: 35
  • WhatsApp Image 2025-04-07 at 19.34.05 (1).jpeg
    WhatsApp Image 2025-04-07 at 19.34.05 (1).jpeg
    219.2 KB · Views: 43
  • WhatsApp Image 2025-04-07 at 19.34.06.jpeg
    WhatsApp Image 2025-04-07 at 19.34.06.jpeg
    565.5 KB · Views: 38
  • WhatsApp Image 2025-04-07 at 19.34.06 (1).jpeg
    WhatsApp Image 2025-04-07 at 19.34.06 (1).jpeg
    611.3 KB · Views: 45
  • WhatsApp Image 2025-04-07 at 19.34.08.jpeg
    WhatsApp Image 2025-04-07 at 19.34.08.jpeg
    634.3 KB · Views: 43
Huyu Mhe. Dishi limeyumba!

Yaani yeye kila kity ni siasa!
 
Waziri aliekuwepo kwenye hii wizara akafanya na ziara hapo somanga wakatuwekea makontena chini ili tupite juu ni nani kwanza
Nauliza tu
 
Ndugu waziri.
Ni lini mtaanza kuwaheshimu wananchi japo kwa kuwapatia taarifa za kweli juu hali inavyoendelea.

Aliyekuwa waziri wa wizara hiyo ambaye sasa yuko mambo ya ndani alitueleza kuwa serikali imetenga fedha katika bajeti ya 2024/2025 ili kufanya ukarabati wa barabara zilizoharibiwa na mvua ya el nino.

Hakuna kilichofanyika sio Lindi na Mtwara tu, bali nchi nzima, hadi sasa mvua nyingine imekuja kutuumbua na leo mnacheza kuwa mtachukua hatua kwa watu wa Tanroads.

Ndugu,waziri wale wanao kaa pale dodoma wakidai ni wawakilishi wa wananchi , wangekuwa wanajitambua serikali ingevunjika.

Maana, waziri na kamati za bunge wanazunguka nchi ka pia , wanashuhudia kinachoendelea lakini hawachuki hatua zaidi ya kupongeza.

Leo waziri anasema atalala site utafikiri ni mlinzi au ana chochote cha kufanya lakini ukweli hausemwi. Waambieni wananchi kwanini miradi imesimama.

Magufuli aliahidi na ikawezekana kuwa mtasafiri kwa "tax"kutoka Bukoba hadi Mtwara. Leo ili usafiri hivyo inakulazimu uongeze na meli au uzungeke mikoa kadhaa kufika Lindi na Mtwara
 
Hela wapige wengine wajenge barabara chini ya kiwango wengine alafu hatua uwachulie wengine uko timamu kweli wewe?
 
Ndio mawaziri wa awamu ya 6 hao lolote linalokuja kichwani ni kufyatua tu
 
Poleni watu wa Lindi. Sema CHURA mwenyewe nina uwakika hajui kinacho endelea uku Tanganyika awepo au asiwepo nchini. Na watoto w mjini wanampangia safari ili wale mpk wapasuke.
KAZI ni kipimo cha utu
 
Back
Top Bottom