Waliosomea fani tofauti na ualimu ndo walimu wa shule binafsi


mkuu umenena.kinachotaki
wa ni serikali kupiga vita hizo mushroom za utitiri wa vyuo vikuu na sio kudharau ualimu. Ofcourse wanacheza na psychology ya soko la ajira lilipo.toka lini mhindi akaendesha chuo? Yeye kazi yake kuuza duka la jumla.serikali yetu nayo imelala maana inakaribisha investors kwenye masuala ya elimu hii si vyema kabisa.
 
Inaonyesha hawa waliosoma fani tofauti wanaujua ualimu vizuri ndo maana wanafaulisha lakn waliosoma ualimu hawajui ualimu ndo maana hawafaulishi

Kazi ya mwalimu si kufaulisha na kufaulu mitihani si kipimo cha mwalimu bora, mwalimu bora ni yule anayemfanya mwanafunzi kuwa na maarifa (It is about how you know not how you pass)
 
Sasa mbona matokeo yakija shule za serikali ovyooooo ndo mnakopangiwa nyinyi huko mliosomea ila pole bana

Kufaulu kwa mtoto kuna mambo mengi yakiwemo mazingira bora ya kusomea na kufundishia, je unaweza kulinganisha na hilo?
 
Kazi ya mwalimu si kufaulisha na kufaulu mitihani si kipimo cha mwalimu bora, mwalimu bora ni yule anayemfanya mwanafunzi kuwa na maarifa (It is about how you know not how you pass)

Kama unajua basi utafaulu.kama hujui hautafaulu.mwalimu anamwezesha mwanafunzi kujua na akijua kitakachofata atakapojaribiwa kwa Mitihani basi atafaulu kwa sababu anajua
 
Hicho kipimo chako unachotumia nacho hakiko sahihi (mitihani) na ndo maana tunapeleka vijana shule kama Mzumbe tukisema ana kipaji maalumu badala ya kusema shule za watoto wenye uelewa mkubwa, hujawahi kumuona mtoto anaweza kuchora vizuri lakini mfumo wetu wa utahini utamuacha nje kwa vile 1 + 1 hawezi??
 

Ni kweli.Ninachokiona hapo ni soko la ajira kwa fani zote kujaa sana.Na hata huo ualimu soko linakaribia kujaa.Miaka michache ijayo hatutajadili fani ipi bora na ipi si bora bali tutajadili kuhusu ni wapi tutapata ajira yoyote ile.Na usharo wa wa-TZ utaisha tu.Maana Engineer wa kitanzania ana jazi ya kushikia wengine viuno na laptop au ipadi mkononi wakati ma-engineer wa kichina wanafanya kazi na degree zao.Unataka/hutaki tufike mahali tukubaliane kuwa waafrika tuna matatizo.Leo hii tusingejadili hapa upungufu wa ajira ya ualimu bali namna ya kuboresha.Tutabaki kulalamika kila siku ooo! Wakenya wanatunyang'anya ajira , lakini hoja ni hii je tunajiandaaje kuboresha elimu yetu.Ualimu sasa ndo mahali pa wakubwa kujipatia umaarufu wa kisiasa. mara naibu waziri wa kilimo kutangaza masuala ya ajira za ualimu.jiulize ni mahala pake?
 
Ifutwe iende wa wapi tatizo sio kufutwa ni kwamba wanafunzi wenyewe awana hata readness ya kusoma so mimi niwafuate nyumbani,pia mshahara unaishia siku3 baada ya kutoka na swala watu kama environmentalist kufundisha geography ni possible tu kwani unafikiri hawa degree holders huko chuo wanajifunza wnayokuja kufundisha akuna hata moja
 
We unafikir aliyeweka hiyo Koz yuko sahihi sana? Nenda shule ambazo wengi wa walimu wake hawajasoma hizo koz unazosema lakini watoto wanafaulu

Na wewe unaandika hapa habari za intruders kufaulisha wanafunzi.Intruders wanajua ku-solve past papers kama short cut .Mwanafunzi akiotea anafaulu,Huo ndio ubora wa elimu?Jiulize kwa nini graduates na wengine wakiomba vibarua wanapewa interviews?Msilete hoja za kutukandamiza walimu hapa! TUPO! TUPO KABISA. Kama hiyo ndio hoja kwa nini mh. Lowasa alikataa mwaliko wa kuhudhuria mahafali ya chuo kikuu kimojawapo hapa nchini? KISA BARUA YA MWALIKO YAKINGEREZA ALIYOLETEWA NA WALE GRADUATES HAKUIELEWA KABISA KINGEREZA KILIKUWA CHA KI-MAIMUNA.KUMBUKA HAIKUWA FANI YA EDUCATION TU.KAMA WENGINE BORA KWANINI BARUA ILIPINDA.SIELEZWI CHOCHOTE GENERALLY ELIMU YETU IMEPINDA KUANZIA CHEKECHEA HADI CHUO KIKUU.NARUDIA TENA KWA FANI ZOTEEE! MSITUSAKAME SISI WALIMU KWA KUJIFANYA NYIE BORA SANA!
 
Mazingira bora ya kusomea acha tuangalia Azania sec school ya Dar es salaam kwanini huwa wanafeli sana kiujumla lkn wapo wanaotoka na point kali vle vle?
Kufaulu kwa mtoto kuna mambo mengi yakiwemo mazingira bora ya kusomea na kufundishia, je unaweza kulinganisha na hilo?
 

Hizo zote ni hasira ulizonazo za kutembea na bahasha muda mrefu, hv ww ni mgeni wa nchi hii? Ukifuata ndoto na wito si utakufa njaaa. Alafu kitu kingine cha kitaalamu zaidi ni kwamba elimu katika nchi yyte ili iwe na manufaa kwa jamii ni lazima itolewe kulingana na mahitaji ya jamii husika si kwamba ww unasomasoma tu chochote unachotaka bila kujali uhitaji wa jamii inayokuzunguka. Kwa sasa Tanzania ina uhitaji mkubwa wa products za elimu kwa waliosomea elimu, fani zote za sayansi na afya ndo maana hata board ya mikopo inatoa kipaumbele kwa hizo fani tajwa. Sasa ww endelea kutokwa povu hyo sociology yako au political science yako eti ndoto utabaki unalialia tu.
 
Unakumbuka kama umesa miaka ya 90 ulifundishwa na walimu wa upe? Hao walimu si walikuwa wanafundisha kwa ubora wa hali ya juu Sana?

Pia definition ya neno UALIMU inasemaje?
 
ha ha ha umeona pro-education wanavyong'aka? Hawataki kuambiwa ukweli. Wanaosoma education wengi wao hawakufaulu vema

we hujitambui! Ulifundishwa na nani? Kama hawakufaulu vema walikufundishaje? Labda uniambie unesomea nje ya nchi.sijui fani yako lakini unaweza ukawa kilaza wa mwisho kwenye hiyo fani.ndiyo! Kwa sababu ulifundishwa na pro - education kama unavyoita asiyefaulu.maskini wewe hujitambui!! Rudi kajiandae urudi upya jukwaani.
 
Sasa Walimu wengi ni arts subjects. Unakuta shule nzima waalimu wa sayansi ni watatu wanne.
 
mbona watu wanasoma sociology na wanafanya kazi bank as bank tellers
wengine wamesoma uhasibu wanafanya procurement...nk!
WALIMU WENGINE MNAPENDA KULALAMIIIIIIIKA....aaaagh, MNATAKA TUWAONE KAMA SPECIAL GROUP, UALIMU NI FANI KAMA FANI NYINGINE BANA
:suspicious::disapointed:
 

sociology na political science ndio mavitu gani??? kwa taarifa yako mi ni biomedical engineer ambaye nimegraduate miaka minne iliyopita!! na hata nilivyorudi Tz sikuhangaika na bahasha kama unavyodai/ unavyofikiria!! nasikia mwakani serikali itaacha kuajiri waalimu labda watakaobahatika ni walimu wa science( hongera kwa walimu wote wa science). nyie wengine mtaungana mitaani na hao waliosoma political science na sociology!! tatizo lenu huwa hamkubali kuwa waalimu wa sasa hamna wito!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…