Waliosomea fani tofauti na ualimu ndo walimu wa shule binafsi

Waliosomea fani tofauti na ualimu ndo walimu wa shule binafsi

Mimi pia nashangaa sana..zamani wakati nipo Advance nilifikiri ni upungufu wa walimu especially science ambayo nilikua naiona sana sababu mm pia nilikua nafanya PCM lakini badae baada ya kuingia chuo nikagundua walimu wapo wengi sana
na bado graduates wa coarse zingine wanaendelea kufundisha mashuleni na sio private tu mpaka government schools!!
 
Kwa vijana wa mjini dar kuna mtu alikua anaitwa mkandawile mkali wa chemistry anafahamika sana kwa tuition pia alikua ni mwalimu wa chemistry kwa A level pugu boys wakati huo mm nilikua O level miaka ya 1997-2000...kama huyu aliwezaje kuwa mwalimu kwny shule ya serikali wakati serikali inajua kuna walimu by professional wanagradute kila mwaka??
 
Mnawadharau sana walimu, Nadhani hii ni kutojielewa.Nyie wote mliosoma kozi nyingine ni product ya walimu.

Tunaweza kusema kama unaona mwalimu ni wa ovyo hata wewe uliesoma fani nyingine pia ni wa ovyo kwani umeandaliwa mwalimu ovyo.

Remember poor teacher produces poor engineer ,doctor,Accountant etc.Jamani niwaelimishe vipi kuhusu umuhimu wa mwalimu ili mnielewe?Hata mwenye akili ya kuvukia barabara tu anaelewa! (Nchi hii elimu itashuka hadi basi hivi vilaza kama nyie mnaodharau walimu kesho mkipata kura za vidole mkawa na nafasi mahala fulani mtaboresha maslahi ya Walimu?

Nchi nyingine wanaheshimu walimu wao nyie mna kazi ya kuwaponda humu jamvini mna laana?
 
NYONGEZA: Kwa uhahika kabisa Serikali iwatoe hawa mamluki waliovamia fani yetu. Tutalipeleka hili suala T.T.U.(C.W.T) Kama hawataki tutawatoa kwa winch. Kama unataka kuwa mwalimu nenda chuoni.!!!
 
NYONGEZA: Kwa uhahika kabisa Serikali iwatoe hawa mamluki waliovamia fani yetu. Tutalipeleka hili suala T.T.U.(C.W.T) Kama hawataki tutawatoa kwa winch. Kama unataka kuwa mwalimu nenda chuoni.!!!

Hahahahhahahha peleka div.3 huko
 
Naomba wizara ya elimu iwachukulie hatua za kisheria wamiliki wa shule binafsi na vyuo vya ualimu kwa kuajili watu ambao hawajasomea taaluma ya ualimu kuwa walimu na wakufunzi wa vyuo vya ualimu. Kitendo hiki kinazidi kinachangia utolewaji wa elimu isiyo bora. Ni aibu kweli kweli unakuta watu wamesomea sociology, Political science, law, engineering n.k eti ndo walimu.

Inaonyesha hawa waliosoma fani tofauti wanaujua ualimu vizuri ndo maana wanafaulisha lakn waliosoma ualimu hawajui ualimu ndo maana hawafaulishi
 
Nimewagusaeee! Naona mnakuja mapovu yakiwatoka mdomoni! Na bado mtajikwaa hata vidole kwa kuelezwa ukweli!!
 
Teh teh ! hatuwezi maana ajira kwetu bado zipo.Wengine wanakwa ajira ndo maana wanakuja!
 
Haya nimekubali karibuni woote! Fundisheni kwa bidii
Tujiandae kupeleka vilaza Kwenye soko la ajira jumuiya ya Afrika mash.Hongera TZ kwa uchakachuaji!
 
Walimu wengi kama siyo wote wa vyuo vikuu hawajasomea ualimu lakini wanapiga kazi nzuri tu.
 
Walimu wengi kama siyo wote wa vyuo vikuu hawajasomea ualimu lakini wanapiga kazi nzuri tu.

yes, hawa wahadhiri wote isipokuwa wahadhiri wa education hawajasomea ualimu. mbona wanafundisha? ukweli utabaki palepale kuwa knowledge transfer haiusiani na hayo mambo ya saikoloji, mitaala na madudu mengine ambayo waalimu wanayasoma huko vyuoni
 
thubutu yao!

mkuu hii ni nchi yetu tunaielewa vilivyo.huko hatuwezi kuja .pamevamiwa siku nyingiiii! Intruders wamejaa huko walimu wala hatuwezi kupata nafasi.ndo maana wanafanya upasuaji wa vichwa badala miguu,ghorofa zinaporomoka kila kukicha.mnashangilia kwetuee! Kwenu ni salamaa?
 
Sasa hii utalinganisha na one mkuu au hujui one manake nini? kwani hujui sheria UDSM inachukua kati point za juu kuliko education? Engineer anaweza kufundisha hata advance math, physics hata chemistry pia
Sasa Div two n ufaulu mdogo?
 
Sasa mbona matokeo yakija shule za serikali ovyooooo ndo mnakopangiwa nyinyi huko mliosomea ila pole bana
Naomba wizara ya elimu iwachukulie hatua za kisheria wamiliki wa shule binafsi na vyuo vya ualimu kwa kuajili watu ambao hawajasomea taaluma ya ualimu kuwa walimu na wakufunzi wa vyuo vya ualimu. Kitendo hiki kinazidi kinachangia utolewaji wa elimu isiyo bora. Ni aibu kweli kweli unakuta watu wamesomea sociology, Political science, law, engineering n.k eti ndo walimu.
 
Unajua ukweli ni kwamba walimu hawataki wengine wafundishe wakiona wanavamiwa ktk kazi zao
Kwa vijana wa mjini dar kuna mtu alikua anaitwa mkandawile mkali wa chemistry anafahamika sana kwa tuition pia alikua ni mwalimu wa chemistry kwa A level pugu boys wakati huo mm nilikua O level miaka ya 1997-2000...kama huyu aliwezaje kuwa mwalimu kwny shule ya serikali wakati serikali inajua kuna walimu by professional wanagradute kila mwaka??
 
Sasa mbona matokeo yakija shule za serikali ovyooooo ndo mnakopangiwa nyinyi huko mliosomea ila pole bana

Vipo vigezo vingi vinavyochangia shule za private kutoa matokeo mazuri.Mojawapo ni idadi ndogo ya wanaf,uwepo wa maabara,usimamizi kwani ni biashara.etc.Uwepo wa intruders kutoka fani nyingine sidhani kama ni kigezo sana!
 
Back
Top Bottom