BARD AI
JF-Expert Member
- Jul 24, 2018
- 3,591
- 8,826
Vijana wawili waliodaiwa kuvamia ofisi ya michezo ya kubahatisha (Premier bet) eneo la Mwenge ITV na kutaka kupora fedha wamefariki kutokana na kipigo walichokipata kutoka kwa wananchi.
Septemba 27, 2022, saa 3:30 asubuhi vijana hao walifika katika ofisi hiyo kama wateja wanaohitaji huduma na kuanza kumshambulia mhasibu kwa kumpiga na jiwe kichwani huku mwingine alijaribu kuvunja shelfu zilizokuwa na fedha bila mafanikio.
Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Jumanne Muliro amesema watuhumiwa hao walifariki baada ya kufikishwa hospitalini.
Amesema kifo chao kinetokana na kipigo walichokipata kutoka kwa wananchi, baada ya kuchoshwa na vitendo vya kihalifu.
"Watuhumiwa wote wawili kwa bahati mbaya baada ya kufikishwa hospital walifariki, baada ya kufuatilia tumebaini kijana mmojawapo alikuwa ametoka gerezani miezi minne iliyopita," amesema Muliro.
Aidha, Kamanda Muliro amewataka watuhumiwa wanaotoka gerezani, kwa kumaliza kifungo au kwa msamaha kufuata sheria na kuachana na vitendo vya kihalifu kwani wananchi wamechoka na vitendo hivyo. Hata hivyo, Jeshi hilo linaendelea na operesheni usiku na mchana.
MWANANCHI