Waliotaka kuiba kwenye ofisi za Betting Dar wafariki dunia

Waliotaka kuiba kwenye ofisi za Betting Dar wafariki dunia

Mob justice, hatuko mbali na yanayotokea hapo SA,sasa police watawatafuta waliofanya hii mob justice?,tunaishi in a shithole country, wapi sheria za nchi?
Ni ajabu hata KAMANDA halaani kitendo cha wananchi kujichukulia sheria mikononi maana hata polisi wake nao wanafanya hivyo hivyo. Kama mahakama zetu zimeshindwa kazi, turuhusiwe tuwaue pia wezi wakubwa serikalini na wabaridhifu wote wanaoiba mpaka "Future" ya watoto na wajukuu wetu. Hawa vibaka na Panya road wanaadhiri mtu mmoja mmoja lakini hao wezi na wabadhirifu wa mali, wana adhiri taifa zima. Kwanini wao tuwaache
 
Vijana wawili waliodaiwa kuvamia ofisi ya michezo ya kubahatisha (Premier bet) eneo la Mwenge ITV na kutaka kupora fedha wamefariki kutokana na kipigo walichokipata kutoka kwa wananchi.

Septemba 27, 2022, saa 3:30 asubuhi vijana hao walifika katika ofisi hiyo kama wateja wanaohitaji huduma na kuanza kumshambulia mhasibu kwa kumpiga na jiwe kichwani huku mwingine alijaribu kuvunja shelfu zilizokuwa na fedha bila mafanikio.

Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Jumanne Muliro amesema watuhumiwa hao walifariki baada ya kufikishwa hospitalini.

Amesema kifo chao kinetokana na kipigo walichokipata kutoka kwa wananchi, baada ya kuchoshwa na vitendo vya kihalifu.

"Watuhumiwa wote wawili kwa bahati mbaya baada ya kufikishwa hospital walifariki, baada ya kufuatilia tumebaini kijana mmojawapo alikuwa ametoka gerezani miezi minne iliyopita," amesema Muliro.

Aidha, Kamanda Muliro amewataka watuhumiwa wanaotoka gerezani, kwa kumaliza kifungo au kwa msamaha kufuata sheria na kuachana na vitendo vya kihalifu kwani wananchi wamechoka na vitendo hivyo. Hata hivyo, Jeshi hilo linaendelea na operesheni usiku na mchana.

MWANANCHI
Unaweza Kuta polisi waliendeleza kipigo baada YA kufika central, Safi Sana raia wamevuna walichopanda.
 
Ni ajabu hata KAMANDA halaani kitendo cha wananchi kujichukulia sheria mikononi maana hata polisi wake nao wanafanya hivyo hivyo. Kama mahakama zetu zimeshindwa kazi, turuhusiwe tuwaue pia wezi wakubwa serikalini na wabaridhifu wote wanaoiba mpaka "Future" ya watoto na wajukuu wetu. Hawa vibaka na Panya road wanaadhiri mtu mmoja mmoja lakini hao wezi na wabadhirifu wa mali, wana adhiri taifa zima. Kwanini wao tuwaache

Viongozi tuliowapa dhamana ya kutuongoza ndio wanaotufikisha hapa,mosi kwa mitahala mibaya ya elimu,pili sheria na sera mbaya mbaya na tatu ukwapuaji wa mamilion ya wananchi unaofanywa na viongozi ingekuwa vyema tuanze kudeal na hawa automatic na huku chini panyaroad nao wangenyooka tu
 
Sasa ndio wamefanyaje jamani hao vijana

Badala ya kubet wao wanakwiba
 
Watu wanahasira za kuliwa mikeka yao, ati vijamaa viwili waje tu kujichukulia kiulani...
 
Back
Top Bottom