Waliotaka kumpiga kwa mawe ili kumwangamiza, wazuiliwa!

Waliotaka kumpiga kwa mawe ili kumwangamiza, wazuiliwa!

Setfree

JF-Expert Member
Joined
Dec 25, 2024
Posts
6,238
Reaction score
8,194
Ni ajabu na kweli. Mji umetaharuki! Tukio hili limewashtua wengi: Mwanamke mmoja amefumaniwa “live” akifanya uzinzi. Wenyeji wamemkamata, wanadai sheria yao inawaruhusu kumpiga kwa mawe hadi afe.

Mambo yamebadilika ghafla! Mwalimu mmoja anayeheshimika sana mjini hapa, kutokana na hekima yake isiyo ya kawaida, amesimama mbele yao na kusema kwa sauti ya utulivu, lakini yenye mamlaka: “Yeyote asiye na dhambi, na awe wa kwanza kumtupia jiwe.”

Duh, ukimya mzito umetanda. Waliokuwa na haraka ya “kumtoa kafara” huyu mwanamke, wanaondoka mmoja baada ya mwingine, kwa aibu, maana wamejitambua na wao wana dhambi.
 
Kwa undani wa habari hiyo ya kweli, soma Yohana 8:1–11
Tukio hili ni fundisho kubwa sana kwetu. Katika jamii nyingi utasikia maneno: "We ni fisadi... we ni mwizi... we ni muuaji... we ni mla rushwa... unadhulumu watu."

Cha ajabu ni kwamba, wanaowashutumu wenzao kwa maneno kama hayo, na wao unakuta ni watu wanaopenda kusema uongo, ni wazinzi na waasherati, ni walevi, ni watukanaji, wanapiga wake zao nk

Katika tukio hilo la mwanamke aliyefumaniwa, Yesu anatufundisha tusiwahukumu wenzetu kabla ya kujitazama wenyewe. Hivyo, kabla hujamnyooshea mwenzako kidole kwamba ni mkosaji, jiulize: Je, wewe huna kasoro? Wewe ni mtakatifu?
Luka 6:41-45
“Mbona unatazama kibanzi kilicho ndani ya jicho la ndugu yako, wala huoni boriti iliyo ndani ya jicho lako mwenyewe? Utawezaje kumwambia ndugu yako, ‘Ndugu yangu, acha nitoe kibanzi kilicho ndani ya jicho lako,’ wakati wewe mwenyewe huoni boriti iliyo ndani ya jicho lako? Ewe mnafiki, ondoa boriti ndani ya jicho lako kwanza, ndipo utaweza kuona dhahiri jinsi ya kuondoa kibanzi kilicho ndani ya jicho la ndugu yako..."
 
Yesu hakusema kwamba yule mwanamke hakuwa na kosa, bali anatufundisha tuwahurumie wenye dhambi, tuwaambie watubu na kuwasamehe - hiyo ndio njia nzuri ya kubadili maisha yao – sio kuwapiga kwa mawe.
Yohana 8:10-11
Yesu akasimama akamwuliza, “Mama, wale waliokuwa wanakushitaki wako wapi? Hakuna hata mmoja aliyekuhukumu?” Yule mwanamke akajibu, “Hakuna Bwana.” Yesu akamwambia, “Hata mimi sikuhukumu. Unaweza kwenda, lakini usitende dhambi tena.”
 
Minaona.....
Nyerere alifanya haraka sana kudai uhuru na kumfukuza mkoloni, ndio maana leo hii tumefika hapa tulipo
 
Sio sawa kumwambia mwenzako "usiibe," wakati wewe mwenyewe unaiba.
Kuna watu wengi leo wanawakaripia wengine, lakini mioyo yao imejaa madhambi yale yale wanayoyakemea! Mtume Paulo aligusia jambo hili kwa ukali. Soma Warumi 2:21

Tuyashushe mawe ya hukumu, tuinue mioyo ya toba na msamaha.

Waliomshutumu yule mwanamke, "walishusha mawe yao"; wakaondoka kimya kimya.
Sasa swali kubwa linabaki: Je, walienda kujitakasa au walienda kutafuta mtu mwingine wa kumhukumu tena?

Habari ya huyo mwanamke inamhusu kila mmoja wetu. Kama maisha yetu sio matakatifu, tuache kuwalaumu wengine kwanini wanafanya uovu. Tuache kuwanyoshea vidole. Tuache kuwapa majina mabaya na kuwahukumu—tujitazame kwanza jinsi tulivyo! Kama maisha yetu sio safi mbele za Mungu, tusifunue kinywa kuwashutumu wengine.
 
Ole ole wako shetani mwanamke, vita na kanisa huwezi.
Hawa sio kama wale unaokula na kunywa nao!
Hawa si kama wale wanao kuimbia na kukusifu!
Na akilala unawakati mgumu
 
Ni ajabu na kweli. Mji umetaharuki! Tukio hili limewashtua wengi: Mwanamke mmoja amefumaniwa “live” akifanya uzinzi. Wenyeji wamemkamata, wanadai sheria yao inawaruhusu kumpiga kwa mawe hadi afe.

Mambo yamebadilika ghafla! Mwalimu mmoja anayeheshimika sana mjini hapa, kutokana na hekima yake isiyo ya kawaida, amesimama mbele yao na kusema kwa sauti ya utulivu, lakini yenye mamlaka: “Yeyote asiye na dhambi, na awe wa kwanza kumtupia jiwe.”

Duh, ukimya mzito umetanda. Waliokuwa na haraka ya “kumtoa kafara” huyu mwanamke, wanaondoka mmoja baada ya mwingine, kwa aibu, maana wamejitambua na wao wana dhambi.
Hivi mbona huyo mwanaume hatajwi sembuse kukamatwa? Hii sio haki kabisa.
 
Ole ole wako shetani mwanamke, vita na kanisa huwezi.
Hawa sio kama wale unaokula na kunywa nao!
Hawa si kama wale wanao kuimbia na kukusifu!
Na akilala unawakati mgumu
Shetani hana jinsia - sio mwanaume wala mwanamke. Halafu LUTULWITU inaonekana huu uzi hujauelewa.
 
Hivi mbona huyo mwanaume hatajwi sembuse kukamatwa? Hii sio haki kabisa.
Hao walikuwa na lengo la kumtega tu Yesu ili wamshitaki. Ukisoma sheria ya Musa, hata mwanaume anatajwa
 
Back
Top Bottom