Pre GE2025 Waliotelekezwa na UVCCM Uwanja wa Mkapa baada ya Tamasha wasaidiwa Nauli

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Erythrocyte

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2012
Posts
128,308
Reaction score
245,426
Zaidi ya vijana 10 miongoni mwa mamia waliotelekezwa Uwanja wa Mkapa baada ya Tamasha la UVCCM lililotumbuizwa na Msanii mpya, ambaye pia ni afisa habari wa Simba Ahmed Ally, wamepita Mbozi Road wakiomba omba hela ya nauli ya kuwafikisha kwao Mwananyamala na Kawe.

Wameingia kwenye ofisi yetu na kujieleza ambako tulimuagiza Mhasibu wetu kumpa sh elfu 5 kila mmoja wao ili wafike makwao, Niliwahurumia sana vijana wale waliovishwa fulana za kijani zenye picha ya Samia, huku wakionekana kuwa na njaa (Hatukuwapiga picha kwa sababu za kibinadamu).

Tunaendelea kusisitiza kwa ccm na idara zake kwamba ni vema wanaposomba watu kuwaleta kwenye matamasha yao wakumbuke kuwarejesha makwao kwa amani.

====

Pia soma: Ni sawa CCM kutumia rasilimali za umma kwa shughuli za chama? Msajili wa Vyama vya Siasa upo tu, au na wewe ni CCM?
 
Iwapo kama watu hao hawakuwa chawa nawapa pole,ila kama wenyewe ni chawa,kawaida ninavyojua chawa stahili yake ni pasi ya moto.Ila kama mliwapiga chawa teke huenda hamkujitendea haki,ila iwapo mlijiridhisha sii chawa basi mlitenda vyama.Kadiri ya matendo ya mtanzania aliye Mzalendo.
 
Habari hii inaonekana inaelea juujuu ni upuuzi mtupu
 
Iwapo kama watu hao hawakuwa chawa nawapa pole,ila kama wenyewe ni chawa,kawaida ninavyojua chawa stahili yake ni pasi ya moto.Ila kama mliwapiga chawa teke huenda hamkujitendea haki,ila iwapo mlijiridhisha sii chawa basi mlitenda vyama.Kadiri ya matendo ya mtanzania aliye Mzalendo.
Kwa kuwatazama tu sidhani kama walijua hata tamasha lile lilihusu nini
 
Kumbe , niliwaona magomeni wakipita na basi huku wakitikisia makalio kwenye madirisha na mbele kioo cha dereva halafu ni vitoto vidogo kabisa.

Nikadhani wanaenda kwenye sherehe na t shirt za kijani kama sare, kumbe ndo walikua wanaenda huko taifa...
 
JANA CCM WALIWABEBA WATOTO WA SHULE KIBAO KWENDA KUWAPELEKA TAIFA WAMEWALETEA BAADHI YA WAZAZI NA WATOTO MATATIZO SANA JANA WAMEJAZA UWANJA WA KUPELEKA MAGARI KUWACHUKUA WANAFUNZI BURE NA KUWAPELEKA KULE TAISHA SO SAD [emoji24][emoji35][emoji56]
 
Zaidi ya vijana 10 miongoni mwa mamia waliotelekezwa Uwanja wa Mkapa baada ya Tamasha la UVCCM lililotumbuizwa na Msanii mpya, ambaye pia ni afisa habari wa Simba Ahmed Ally, wamepita Mbozi Road wakiomba omba hela ya nauli ya kuwafikisha kwao Mwananyamala na Kawe.

Wameingia kwenye ofisi yetu na kujieleza ambako tulimuagiza Mhasibu wetu kumpa sh elfu 5 kila mmoja wao ili wafike makwao, Niliwahurumia sana vijana wale waliovishwa fulana za kijani zenye picha ya Samia, huku wakionekana kuwa na njaa (Hatukuwapiga picha kwa sababu za kibinadamu).

Tunaendelea kusisitiza kwa ccm na idara zake kwamba ni vema wanaposomba watu kuwaleta kwenye matamasha yao wakumbuke kuwarejesha makwao kwa amani.

====

Pia soma: Ni sawa CCM kutumia rasilimali za umma kwa shughuli za chama? Msajili wa Vyama vya Siasa upo tu, au na wewe ni CCM?
Mkuu kama kuomba ni dhambi mbona lissu anaomba!
 
Back
Top Bottom