Waliowahi kutolewa majini/Mashetwani

Njoo nikuoneshe jamaa anaitwa SHAGIRA aliyekuwa kichaa kabisa tangu namfahamu, yaani inazidi miaka 7...leo nimemkuta Hardware ananunua PVC pipes

Kuuliza nikaambiwa aliombewa nyumbani na mchungaji akapona

Ni leo hii ninemwona
 
Kwa maoni yangu naona bado una nafasi ya kuendelea kutafuta tiba hospitali, binafsi sijaona sababu ya kufanya uhisi una jini bado naona ni changamoto tu za kiafya ila kama unasisitiza kuwa una jini basi ni vyema upate mtaalamu wa kuangalia kwanza tatizo ni nini kama ni kweli jini,uchawi au ni tatizo tu la kiafya.
 
Mpokee YESU KRISTO awe Bwana na Mwokozi wa maisha yako!

Waganga watakutapeli hela, watakulisha hadi vinyesi kisha watakuchanja chale hadi makalioni na usipone!
Una ushaidi? Acheni ulokole kwenye mambo ya seriously.
 
Tafuta sheikh mkuu hayo mavitu yanatoka fasta sanaa.
 
Imeandikwa ...mpingeni shetani naye atawakimbia...
Ukaombewe mapepo/majini hutoka kabisa nimeshuhudia mara nyingi nyingi mnoo
 
You definitely need help my broda
 
Tatizo kuna wataalamu wanaongea nayo lugha moja na wanatumia kitabu kimoja

Wanafanya nayo negotiations na kuyabembeleza kwa kitu wanachokitaka na mwishowe yanatoka yake madogo lile lililokubuhu anakuambia HILI LITAKUWA LINAKULINDA

Dalili za wazi za mtu anayeishi nayo ni kitoa sauti kama anabeua au anavuta hewa kwa nguvu inagomea kwenye koo na kutoa sauti, wengi ni wanawake
 
Hivi matajiri kama Mo au Bakhressa na hata Elon Musk,wanapatwaga na hayo so called mashetani?
Hata kwenye kuombewaombewa sijawahi kuwashuhudia kwakweli.
 
Hivi matajiri kama Mo au Bakhressa na hata Elon Musk,wanapatwaga na hayo so called mashetani?
Hata kwenye kuombewaombewa sijawahi kuwashuhudia kwakweli.
Hata akipata wale wana Waganga wakubwa. Chawa wake huwapelekea wataalum nyumbani kwao.
Na ole wako akufahamu mhusika. Una tangulia mbele ukamsalimie JPM. Hivyo maadaui wa ki puuzi hawana. Wana ondolewa fastaaa.

Maskini ukiombwa mil 6 jamaa adunguliwe huna.
 
Mmmh...! ntafanya utafiti nijiridhishe.
 
Hv majini yanawaogopea nn matajiri na kuwaonea masikini tu. Sijawahi sikia hizo swaga za majini kwa matajiri Wala nn
 
Wanatoka kabisa, kwa maombi, unaishi wqpi?
 
Hv majini yanawaogopea nn matajiri na kuwaonea masikini tu. Sijawahi sikia hizo swaga za majini kwa matajiri Wala nn
Mkuu hawa matajiri hukumbwa na kadhia hii ,hasa kwa watoto wao n.k ,lkn huwexi sikia sababu haya mambo huyafanya siri na kuyatatua kimya kimya ,tofauti na sisi waswahili mtu akiumwa tunapitisha bakuli kwa ndgu jamaa na marafiki ndomana taarifa zinazagaa ,ila kwa matajiri hufanya mambo yao kimya kimya na kwa siri hata kwa mtaalam ,au shekh au padri huwa wanakuwa na mlango wa vip ,huwakuti wakipanga foleni kama sie
 
Pole Sanaa Mkuu jiandae kuwa Mtabibu
 
Hivi matajiri kama Mo au Bakhressa na hata Elon Musk,wanapatwaga na hayo so called mashetani?
Hata kwenye kuombewaombewa sijawahi kuwashuhudia kwakweli.
Matajiri huwezi kuona au kujua mambo yao mengi tu mkuu.
 
Hv majini yanawaogopea nn matajiri na kuwaonea masikini tu. Sijawahi sikia hizo swaga za majini kwa matajiri Wala nn
Tatizo ni kufikiri tajiri ni sawa na wewe na chengine vitimbi au athari za majini sio lazima ziwe za kukuingia mwilini au kupata maradhi.
 
Hizo zote ni dadili za kuingiliwa katika mwili wako. Fanya hima kumpata mtumishi wa kweli wa Yesu Kristo akusaidie manake madude hayo yanatesa sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…