Lady Mwali
Senior Member
- Nov 15, 2018
- 147
- 333
Wanabodi,
Siku za nyuma niliweka thread kuhusu mauaji ya kijana Jumanne Jongo kuuawa na sungusungu maeneo ya Beach Boy Mburahati.Kijana huyu anaishi maeneo ya Banda Mabibo.
Kijana aliyeuawa anaitwa Abdu ana umri wa miaka 19.
Kilichotokea ni kwamba kijana aliyeuawa alikwenda kwenye mziki maeneo ya Banda.Huyu kijana anakaa maeneo ya Bongo Beach alipouawa Jumanne Jongo.
Baada ya kufika katika mziki huo kwenye sherehe ya ushindi wa bondia wa Banda, mabaunsa walimuona huyo kijana wakaanza kumshambulia kwa kumpiga visu maeneo mbalimbali ya mwili,kooni,tumboni na kichwani.
Kijana alifia hospitali ya Mwananyamala baada ya kuvuja damu nyingi.
Sungusungu walichukua sheria mkononi kwa kuua kijana Jongo
wahuni wa Banda nao wamelipiza kisasi kwa kumuua huyu kijana anayehisiwa yeye au baba yake walihusika katika mauaji ya Jongo kwa kivuli cha
sungusungu.
Hii inatokana na uhasama mkubwa uliopo kwa wakazi wa maeneo haya dhidi ya sungusungu.
Hatujui atafata nani, ila hao sungusungu wa Jitegemee na Mburahati waache kiherehere kwani wako hatarini kushambuliwa na hawa wahuni wa Banda na kuuawa.
Kuna haja kuwe na upatanisho kati ya sungusungu na vijana wa Banda, bila hivyo maafaa yatatokea zaidi.