Walitakiwa 'Wa-jembe';si Wajumbe!

VUTA-NKUVUTE

JF-Expert Member
Joined
Nov 25, 2010
Posts
6,137
Reaction score
17,908
Hakuna kukosea.Hakuna kubahatisha. Kila kitu ni mipango. Mipango asubuhi,jioni mahesabu. Ndivyo alivyofanya Mwenyekiti wetu, Ndugu Jakaya Mrisho Kikwete. Ameteuwa 'Wa-jembe' wa Katiba. Amehakikisha kuwa maandalizi ni ya kuvutia kupitisha kila hoja na msimammo wa chama chetu cha Mapinduzi. Mwenyekiti ametisha. Rais halazimishwi kufuata tafsiri za watu Sheria inayosimamia Bunge la Katiba.

Makada machachari na 'waliokunywa maji ya bendera' wakiongozwa na Mzee Kingunge Ngombare Mwiru ni wa muhimu katika Bunge hilo hasa kwa upande wetu. Ni mfano wa Wa-jembe wa Katiba.Yuko pale kwa ajili ya kutengeneza njia ya kupitisha hoja za kichama. Yeye si 'Mjumbe'. Ni M-jembe (kwa kutengeneza njia).

Ndiyo maana kuna usanii ilibidi utumike. Wateuliwe kimtindo.Kutoka katika kundi 'tata' la watu wenye malengo yanayofanana. Kwakuwa hakuna tafsiri rasmi juu ya kundi hilo,na wala haikuhitajika, Mwenyekiti ameteua Wa-jembe wote 'kihalali' kabisa. Wapo wasio na hata NGO wala Shirikisho lolote.Lakini,wana malengo yanayofanana: kupitisha maoni na msimamo wa chama bila kikwazo. Wa-jembe!

Kazi yao itonekana Bunge la Katiba likianza. Mtajionea.Mtafurahia.Sasa roho zetu zimetulia. Tuna uhakika.Uhakika wa ushindi wa kimbunga. Mnaotaka uteuzi wa Wajumbe wa Bunge la Katiba mtatusamehe. Chama kwanza, nyinyi baadaye!

Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam

 
Ndicho hasa alichofanya mkuu wa kaya.Nimeshangazwa sana kusoma jina la mwanasiasa na mwanahabari kwenye kundi moja,ama mama Shamim Khan kwenye kundi la viongozi wa dini.Nilishangaa pia mzee Kingunge kuwa kwenye kundi la wanaowakilisha asasi za kiraia.....Ama kwa hakika mkuu wa kaya hana nia njema na taifa hili.
 
Mwenyekiti hakukosea

Mzee Tupatupa wa Lumumba
 
huyo hajali kitu anahitaji kuchenshwa sana
 
Hili la katiba ni kiini macho hapa wapizani waweke mitego yao kwenye kura ya maoni .. Nipo mbali na bongo kidogo ila mambo yananiuma kweli
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…