Bado mnaweweseka na rank za IFFHS tu? wakati hao hao IFFHS walipoweka rank kuwa Simba ipo juu zaidi ya Sevilla mbona hamkufungua nyuzi nyingi za kuwaponda IFFHS?
IFFHS ina deal na namba tu ndio maana wanaitwa international federation of football history and statistics, wanachokifanya wao ni kupima performance za timu katika michezo yote ya kimashindano wanayocheza yaani ya kitaifa na kimataifa. Wao wana record kila aina ya data inayohusiana na performance za timu mfano idadi ya clean sheets, idadi ya mechi ilizoshinda, idadi ya magoli ya kufungwa, idadi ya magoli yakufunga, n k kila data inachukuliwa katika mechi za ligi kuu, FA na mashindano ya kimataifa.
Narudia tena IFFHS wanapima performance za timu kwa mashindano yote anayoshiriki kitaifa na kimataifa (kila mwanachama wa shirikisho la soka lazima awe na mashindano ya ligi kuu na FA) tofauti na ilivyo kwa shirikisho la CAF wao wana deal na mafanikio ya timu katika mashindano ya CAF