Lord denning
JF-Expert Member
- Jun 3, 2015
- 15,819
- 33,255
Hakuna marefu yasiyo na ncha.Huu ni msemo wetu wa kiswahili ambao una maana pana sana.
Siasa za kusini mwa jangwa la Sahara zimeanza kuchukua njia ya tofauti kabisa siku za karibuni. Vyama vilivyopigania uhuru kwenye nchi za kusini mwa Afrika vimeanza kukabiliana na vuguvugu la mageuzi.
Vuguvugu hili limeanzia Afrika Kusini ambapo baada ya kuongoza kwa miongo mingi chama cha ANC hatimaye kilitingishwa kwenye uchaguzi mwaka huu uliopelekea wakubali kuunda Serikali ya mseto. Mageuzi haya yalienda hadi Botswana ambapo chama tawala kilichoongoza kwa miongo mingi kilishindwa uchaguzi na chama cha upinzani.
Nchini Msumbiji napo hapajapoa. Saivi kuna vurugu kubwa zinaendelea kutokana na chama tawala kupindua uchaguzi.
Kilichofanyia Msumbiji ndicho wanachofanya CCM nchini Tanzania. Yaaani wananchi nendeni mkapige kura na haijalishi mmemchagua nani kwa kura zenu, kikundi kidogo cha watu wachache kitawaamulia nani ndiye mshindi kwenye huo uchaguzi na sio kura zenu.
Suala hili lilithibitishwa na aliyekuwa Waziri wa mawasiliano Bwana Nape Nnyauye kuwa anayetangaza mshindi ndiye anayeamua uchaguzi na wala sio kura za wananchi.
Baada ya kutokea yanayotokea msumbiji baada ya wananchi kusema hapana na kuamua kuingia mtaani, swali langu ni Je, wananchi wa Tanzania wataweza lini kusema hapana kwa udhalimu wa CCM?
Je ncha ya Chama cha Mapinduzi itakuwa lini? Wananchi wa Tanzania wataendelea kuwa makondoo kama walivyoonyesha ukondoo wao kwenye uchaguzi wa Serikali za Mitaa juzi kati?