Wadau habarini? Kuna watu wasema wanamiliki simu za mikopo kutoka kampuni ya Airtel. Lakini kwa siku mbili zilizopita hawapati huduma. Wanalipa pesa lakini hawafunguliwi.
Wakipiga simu kutaka kujua tatizo nini, simu zao zinakatwa. Sasa wanasema bora wakaziflashi tu ili waendelee kupata huduma ya mawasiliano. Wanasema leo (15/ Agosti 2025) ni siku ya 7.
Mmiliki mmoja wa simu hizo anasema anapiga simu kwa namba ya kawaida ambayo huwa akichelewa kulipa deni ndiyo kampuni inatumia kumpigia kumkumbusha, haipokelewi au inakata! Akipiga Huduma kwa Wateja (customer care) 100 pia haipokelewi au inakata.
Mimi nawaambia Airtel taarifa hii ili mshughulikie tatizo hili haraka. Wako wateja wenu licha ya kulipa madeni ya siku husika lakini mmefungia simu zao, hawako hewani!!