Sesten Zakazaka
JF-Expert Member
- Sep 10, 2017
- 10,559
- 19,101
Habari za Jumamosi Wanamichezo wenzangu
Nimeshangazwa sana na kitendo cha Rais wa TFF kwenda kugombea na hatimaye kuukwaa Urais wa Shirikisho la Vyama Vya Soka kwa nchi za Afrika Mashariki na kati yaani CECAFA. Nimewashangaa zaidi wajumbe waliopiga kura kupitisha hilo!!! Najiuliza ni kwa lipi hasa alilofanya kwenye soka la Tanzania kiasi kwamba aonekane anasifa za kuiongoza CECAFA na alete mapinduzi ya fikra juu ya undeshaji wa shirikisho hilo kwa manufaa ya soka la ukanda huu
Huyu ni mtu ambaye ameshindwa kuboresha uendeshaji wa soka la hapa Tanzania ikiwemo kushindwa hata kuipatia udhamini ligi kuu ya nchini mwetu kiasi kwamba vilabu vidogo vinaumia sana na hivyo kwa kiasi fulani kufanya uwanja wa kiushindani kwenye ligi usiwe sawa
Kina Nicholas Musonye walimfanyia figisufigisu aliyekua katibu Mkuu wa wakati huo Bwana Sam Obingo ambaye alifanikisha mambo mengi makubwa kwa Shirikisho na wakamtoa, matokeo yake CECAFA imekua kama chama cha kuendesha ma bonanza ya vilabu na timu ya Taifa. Imefikia hatua sasa kwenye Senior Challenge Cup mshindi hapati zawadi ya pesa na badala yake washiriki ndio wanatakiwa kulipa Dollar elfu ishirini ili kuingia kwenye mashindano!!!
Uroho wa madaraka ya kupigiwa kura ndio umesababisha Karia aengie huko akiwa hana mkakati wowote wa kumarisha CECAFA! Utabiri wangu ni kwamba anaenda kuizika kabisaa! Sijawahi kumkubali huyu jamaa kupewa uongozi kwa level ya Urais sio tu wa CECAFA bali hata TFF yenyewe