Wallace Karia na RC wa Tabora, Paul Chacha kuwa wageni maalum kwenye mechi ya Simba SC dhidi ya Al Masry

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
5,383
Reaction score
18,776
Klabu ya Simba SC imemtangaza Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Wallace Karia, kuwa mgeni maalum katika mchezo wa mkondo wa pili wa robo fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika (CAFCC) dhidi ya Al Masry. Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa Aprili 9, 2025 kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.

1743764035130.png
Akizungumza leo Aprili 4, 2025 katika uzinduzi wa kipaza sauti maalum (Kispika), Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Simba, amesema:

"Mgeni maalum wa mchezo wetu wa robo fainali dhidi ya Al Masry ni Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya CAF, Rais wa CECAFA na Rais wa TFF, Wallace Karia. Tuna kila sababu ya kumpa nafasi hii kwa kutambua mchango wake. Simba SC kufika nafasi ya sita kwa ubora Afrika ni katika uongozi wake."

1743764115006.png
Mbali na Karia, klabu hiyo pia imepanga kumwalika Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Paul Chacha, kushuhudia mchezo huo muhimu.

"Tunafanya utaratibu wa kumwalika Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Paul Chacha, aje kujumuika na Watanzania kuangalia mwakilishi wa nchi anavyopambana kuingia nusu fainali. Tunamwalika kwa sababu ya mchango wake katika kuhamasisha michezo na pia ajifunze maandalizi ya kimataifa kwa ajili ya kuiandaa timu yake ya Tabora United."

1743764214559.png
​
 
Kwenye hiyo tarehe atskuwa bado ni RC!
 
na kwenye derby waje pia wawashuhudie mnavyokimbia kipigo!
 
Wananchi tunafurahi sana kuona watu wenye midomo mirefu wakiteseka.
 
Rais Samia ikimpendeza amteue Paul Chacha kuwa RC wa muda wa Dar es Salaam kuanzia sasa hadi baada ya tarehe 9 ili awashughulikie wale watakaoleta viherehere kwenye shughuli isiyowahusu.
 
Back
Top Bottom