Wallace Karia ndio Rais wa TFF mwenye mafanikio zaidi katika soka la Tanzania

Hakuna mtu hapo. Rais wa ukweli wa TFF atabakia daima kuwa Leodgar Chilla Tenga. Na siyo hao wanasiasa maslahi wa kulea vitambi tu.
Tenga amefanya nin kumzid Wallace? Tufanye comparison wa ligi yetu kipindi cha Tenga na Wallace..
 
Uto watakwambia ni Jamal Malinzi aliekwenda mtaani kukusanya wachezaji ili kuunda timu ya taifa. Uto ni uto tu.
😂😂😂 Hivi kweli Ile akili waliipata wapi ? Yaani mchezaji wa timu ya taifa ukamtafute vijijini 😂😂😂
 
Acha mihemuko naamin una elimu nzuri, usifuate mkumbo hebu tulia na tumia akili yako, simba imebebwaje na Karia?
Aaaaaah!!! Kwamba hujui Karia anaibebaje Simba. Najua unajua ila hutaki tu. Hata juzi dhidi ya Singida ni dhahiri refa alipewa maelekezo na ukitaka kuamini subiri kama kuna hatua itakayochukuliwa kwake.

Au isije wewe ni Karia !!!
 
Hapa utopolo hawakuelewi Maana huwa Wana chuki binafsi na huyu mzee hata kama angefanya mazuri kiasi gani
 
Tenga amefanya nin kumzid Wallace? Tufanye comparison wa ligi yetu kipindi cha Tenga na Wallace..
Wewe fanya tu hiyo comparison kwa wakati wako. Ila mimi nitaendelea kumtambua Leodgar Tenga kama rais bora kabisa wa TFF kuwahi kutokea mpaka sasa.

Na hata hapa nilipo, natamani kuona wakati mwingine TFF inaongozwa na wachezaji wastaafu, na siyo hawa wanasiasa mamluki kutoka CCM.
 
Aaaaaah!!! Kwamba hujui Karia anaibebaje Simba. Najua unajua ila hutaki tu. Hata juzi dhidi ya Singida ni dhahiri refa alipewa maelekezo na ukitaka kuamini subiri kama kuna hatua itakayochukuliwa kwake.

Au isije wewe ni Karia !!!
Ama kweli shukurani za punda ni mateke. Karia huyu aliyeibeba Yanga kwa kumfanya GSM kuwa mdhamini mwenza wa ligi kuu huku akiidhamini Yanga ili tu Yanga angalau iambulie ubingwa baada miaka minne kupita leo mnamsimanga?
 
Naheshimu mawazo yako mkuu, yatabaki kuwa mawazo yako na sio hali halisi.
 
Ama kweli shukurani za punda ni mateke. Karia huyu aliyeibeba Yanga kwa kumfanya GSM kuwa mdhamini mwenza wa ligi kuu huku akiidhamini Yanga ili tu Yanga angalau iambulie ubingwa baada miaka minne kupita leo mnamsimanga?
Haaahaaa!!!! Haaahaaa!!!! Kwamba Karia ndio kampeleka GSM Yanga
 
Lakini kuna mapungufu ya kizembe ya waamuzi wala hayahitaji yeye kuyasimami ambayo ndiyo msingi wa haki ya mchezo kupata matokeo sitahiki
 
Sio kweli, ukiona mambo yanaenda popote ujue kiongoz wa juu ni mwajibikaji. Tuache unafiki pemben jamaa amefanya makubwa. Utaona siku akiondoka
Tenga aliingia TFF mwaka 2004, alibadilisha sana Ligi yetu, udhamini, na kila kitu, yy ndio alifanya hata TAIFA STARS ikubalike na Jamii. Tenga ndio alifanya hata wadhamini waanze kujaa kwenye Ligi kuu na hata Taifa Stars, Serengeti Boys nk.
Ligi ilikuwa yenye ushindani, na kila timu ilipata vifaa vya michezo kutoka kwa mdhamini nk.

Karia amekuta tayari kila kitu kiko sawa, AZAM TV wapo, Vodacom walikuwepo, na vitu kibao, amekuta mafanikio tayari.
 
Alivyotoka Tenga si walikuwepo akina Malinzi, walifanya nin?
 
Mmeshalegea
 
Ukisikia matatizo ya akili ndo hayo sasa, ligi haikuwa na mdhamini? Mkataba na Azam aliuleta Karia?
Usingeweka neno "matatizo ya akili" hoja yako ingekuwa na mantiki zaidi, Anyway Terms za mkataba wa Malinz na Azam then Karia na Azam zinafanana? Unadhan kwanin Karia ameweza kumodify zaidi mkataba?? Kwanin ameaminika?
 
Ukisikia matatizo ya akili ndo hayo sasa, ligi haikuwa na mdhamini? Mkataba na Azam aliuleta Karia?
dalili namba moja ya mtu kushindwa hoja ni kutumia kauli zisizo za staha na hapa ndipo unapodhihirika UNYANI wa mashabiki wa utopolo kama alivyosema SIR LUC EYMAEL.
 
Usingeweka neno "matatizo ya akili" hoja yako ingekuwa na mantiki zaidi, Anyway Terms za mkataba wa Malinz na Azam then Karia na Azam zinafanana? Unadhan kwanin Karia ameweza kumodify zaidi mkataba?? Kwanin ameaminika?
Terms zinabadilika kutokana na muda, so sio hoja yenye mashiko. Ndio maana kuna kitu kinaitwa Time Value for money. Si umeona ukarabati wa uwanja wa Taifa ni bil 30 wakati ujenzi wake wakati huo ulikuwa bil 60?

Tunachozungumzia hapa ni mafanikio yaliyoleta changes za mpira wetu. Katika hilo Tenga amemuacha mbali KARIA, ni sawa na kumlinganisha Magufuli na Mkapa. Mkapa hakuweza kujenga barabara kila mkoa ila kwa wakati wake ndio alitengeneza mifumo madhubuti na kuwa turning point ya TZ kuwa nchi inayotazamika.

Hata Uingereza pamoja na Maendeleo ila historia yao inaonesha kuwa Agrarian na Industrial revolutions era ndio zama bora kwao katika maendeleo ya nchi yao.

So kwenye Mpira, turning point yetu ni Tenga, enzi zake ligi kuu ilipata kuoneshwa na GTV ambaye alikuwa mshindani wa SUPER SPORTS, Enzi za Tenga, Ligi ilikuwa inachezeshwa angalau kwa ufanisi licha ya kutorushwa game zote.

Uwazi katika Taasisi ulianza kuonekana kipindi cha Tenga, na hata mashindano mengi ya CECAFA yalifanyika TZ kipindi cha TENGA.

Karia amekuta tayari Soka letu liko kwenye Ramani yeye ameingia 2017, ni juzi tu hapo, tayari timu kama Yanga ilishaingia Group stage ya Shirikisho nk ameikuta Taifa Stars tayari ina watu wa maana kuweza kupambana na kufuzu AFCON nk.

Amekuta Karume imefanyiwa maboresho nk.

Kama hujui mpira au una mahaba au ni kampeni meneja wake, mwambie muda ukiisha aondoke ofisini haraka sana. Hakuna ambacho amefanya kwa ufanisi zaidi ya kuwafungia watu.
 
Una hoja yes, hizo raman ambazo Tenga aliziacha mtu wa kwanz kuzikuta na kuanza nayo ni Malinz, alikaa ofisin almost 4 years (2013-2017) lakin hatukuona program zozote za timu iwe za Taifa au Vilabu, thaman ya ligi yetu bado haikuwa na tija, so ishu sio msingi uliowekwa, hapa suala ni nani ameukuta huo msingi na juu yake ameweka nin, leo ligi yetu ina mvuto na thaman kwasababu ya uongoz thabit wa TFF chini ya Karia.

Hata km Tenga aliweka foundation nzuri lakn kwa viongozi wa ovyo km Malinz still tusingefika popote, so still hoja yangu inasimama kwamba Karia ni Rais bora zaid.

Tenga amekaa ofisin miaka 10, ni kweli kuna mazuri ameyaweka na soka letu likaanza kuwa na tija, lakin tunabaki pale pale hajafikia mafanikio ya Karia. Tukichukua mafanikio ya Tenga kt miaka yake 10 ya Uongoz na Karia kt miaka yake 6 ya Uongozi, Karia ana mafanikio zaidi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…