SAYVILLE
JF-Expert Member
- Mar 25, 2010
- 7,895
- 12,975
Embu tuwe wakweli kidogo, jumuisha Marais wote wa Nchi, Mawaziri, Manaibu Waziri, Makatibu Wakuu wa Wizara, Marais na Wenyeviti wa TFF na FAT, hakuna hata mmoja ukichukua mafanikio ya mpira nchini katika kipindi chake ambaye anamfikia Wallace Karia.
Sikubaliani na kila anachofanya au kilichofanyika katika kipindi chake cha uongozi ila kuna mengi mazuri ya kujivunia ambayo yamefanyika.
Leo hii timu zetu za taifa zinaenda sehemu mbalimbali duniani bila wasiwasi na zinarudi na makombe. Kwa watoto wa 2000 wasiojua, kuna kipindi timu zetu zilikuwa zinashindwa kusafiri inabidi kamati ziundwe zichangie pesa.
Vilabu hasa vya Simba na Yanga vimekuwa tishio katika mashindano ya CAF hadi tumeanza kuyachukulia poa mafanikio yao.
Mpira wa wanawake umekua sana na naamini nguvu ikiongezeka kule wanawake wengi sana watafaidika kupitia mpira, na hapa naongelea chain nzima kuanzia kwenye uongozi, ufundi, uchezaji na maeneo mengine.
Ubora wa viwanja vinavyotumika katika ligi kuu nao hakuna anayeweza kubisha katika hilo.
Hapo sijaongelea Maafisa Ubashiri waliotapakaa nchi nzima wanaotimiza ndoto zao za kuwa mabilionea, mkeka mmoja at a time.
Big up sana kwake.