Wallace Karia simama imara. Kuna watu wanakusaka kila pembe ili mradi tu

Wallace Karia simama imara. Kuna watu wanakusaka kila pembe ili mradi tu

AbuuMaryam

JF-Expert Member
Joined
Dec 26, 2015
Posts
2,577
Reaction score
4,637
Kinachoendelea ni kwamba kuna genge linaloongozwa, au kama si kuratibiwa na (Mdau mmoja wa michezo mkubwa kutoka radio iliyoko Maeneo ya DARAJANI Barabara ya KAWE).

Kwa kutumia watu wanaopatikana au kwa mgongo wa club moja kubwa hivi hapa nchini yenye jina la Mnyama wa Pori.

Wanatumia kila mbinu na chokochoko kuichafua na kuipuuzisha kama si kuisahalausha kazi NZURI iliyofanywa na WALLACE KARIA katika uongozi wake...

Tuwe wa wazi tu baada ya CHILA TENGA hakuna uongozi wa TFF uliofanya mengi makubwa kwa mpira wa bongo kama sio huu wa KARIA...amefanya kazi kubwa isiyohitaji kubezwa....

Ndio maana kuna genge la wahuni linaloongozwa na huyo bwana mwenye asili ya Mahali ilipotokea ajali ya MV BUKOBA...kuzusha chokochoko yoyote ili mradi LAWAMA na SHINIKIZO liende kwa KARIA kujiuzulu...

Kuhusu hili la GSM, aliyelianzisha na kumshauri CEO wa CLUB hiyo ya MNYAMA aupinge na kuzusha kahoja kepesi ka FAIR COMPETITION ambayo kwa namna yoyote isingekuwa hivyo walivyosema yeye na GENGE lake, ila lengo ni KUHARIBU MCHAKATO MZIMA UTAKAOZISAIDIA VILABU KUJIENDESHA ili ionekane na lawama ziende kwa uongozi kwa kushindwa kuwezesha vilabu vingine vya ligi kuu KUJIENDESHA na kuweza kushiriki vema ligi kuu.

Hasara ni kwa vilabu vingine ukiacha YANGA, SIMBA na AZAM zitaathirika sana mgogoro huu wa kimaslahi ya watu wachache kama huyu BWANA na genge lake.

Kama KARIA asipochukua hatua za haraka kulidhibiti genge hili...basi watakurudisha nyuma na kukuchafua...sio kwa lengo la kujenga, BALI NA WAO WAPATE KUINGIA NAO WALE KEKI YA MPIRA.

Kwenye suala la GSM, ni WAZI kuna masuala ya kimkataba mbali kabisa na suala Simba kutokubali kuvaa nembo ya mdhamini, ambayo hayo ndio yaliyochelewesha PESA kupelekwa kwa vilabu kama walivyokubaliana...na sababu hiyo hiyo ndiyo waliyofanya wajitoe...

Nakaribisha MJADALA...

NJE YA MADA KIDOGO:
Mbona suala la V.A.R tunali COMPLICATE hivi...tufanye kadri ya uwezo...

mbona tukiwa tunaangalia mpira kwa TV inakuwa ni haraka sisi tunaona REPLAY ya matukio ya uwanjani ..hivi haiwezekani kwa AZAM wakatuwekea ka TV ka Inch hata 55" pale uwanjani kanaonesha mechi kwa mwamuzi wa akiba ili amshtue mwenzake wa ndani kama uamuzi wowote labda hakuoona vizuri.

TUFANYE KADIRI YA UWEZO WETU.
 
We ni WA kupuuzwa, haikuwa sahihi GSM kuizamini Club ana vilabu vingine kama 3 hafu akazamini na ligi, hapo hakuna fair competition kama alitaka angezamini usambazaji wa jezi za timu
 
We ni WA kupuuzwa, haikuwa sahihi GSM kuizamini Club ana vilabu vingine kama 3 hafu akazamini na ligi, hapo hakuna fair competition kama alitaka angezamini usambazaji wa jezi za timu
SAWA SHABIKI WA SIMBA...UMEONEKANA...
 
SAWA SHABIKI WA SIMBA...UMEONEKANA...
IMG-20220207-WA0027.jpg
 
Huu utopolo nadhani umeuandika ukiwa umebanwa kinyesi matakoni. Hakuna anayekataa udhamini katika ligi yetu. Kinachopingwa na wadau ni ule ujanjaujanja wa mkataba wenyewe wa udhamini.

Uliona wapi mkataba wenye mashart ya kutohojiwa na mtu unaemdhamini? Huo ujinga uko huko utopoloni tu. Simba hakuna mazuzu wa namna hiyo wa kutohoji pale wanapoona inafaa kufanya hivyo.
 
Naona Gongowazi wameumia sana kuliko TFF na Bodi ya Ligi.

Haya mwiba wa koo umekwama kuutoa sasa.
 
Huu utopolo nadhani umeuandika ukiwa umebanwa kinyesi matakoni. Hakuna anayekataa udhamini katika ligi yetu. Kinachopingwa na wadau ni ule ujanjaujanja wa mkataba wenyewe wa udhamini. Uliona wapi mkataba wenye mashart ya kutohojiwa na mtu unaemdhamini? Huo ujinga uko huko utopoloni tu. Simba hakuna mazuzu wa namna hiyo wa kutohoji pale wanapoona inafaa kufanya hivyo.
Naweza nikahoji mkataba wako wa kazini?
 
Ila jamaa akili zako fyatu sana!! Sijui kwa nini utoh hamna akili za kufikiri.. unaweza kuta hapo wewe msoni Kabisaa wa degree au masters lkn unachoandika unaweza ukafikiria mara mbilimbili kama either akili umeazimisha au tu basi ndo ulivo..

Eti kalia achukue hatua za haraka adhibiti genge hili .. utafikiri karia mwenyewe ana dola ya kufanya hivyo... karia mwenyewe kapata mafanikio chini ya mgongo wa simba halafu leo eti adhibiti simba.... .
 
Tangu Magori ambaye alimuingiza Chaka Mudy na Simba katika usajili aone anakwenda kuaibika kwa matokeo ya uwanjani amekua akitafuta sababu za nje ya uwanja. Ila shida iliyopo Timu ya Simba imesha haribika na hakuna Namna wanaweza repair damage aliyo sababisha .Awe mpole asubiri msimu ujao
 
Kinachoendelea ni kwamba kuna genge linaloongozwa, au kama si kuratibiwa na (Mdau mmoja wa michezo mkubwa kutoka radio iliyoko Maeneo ya DARAJANI Barabara ya KAWE).

Kwa kutumia watu wanaopatikana au kwa mgongo wa club moja kubwa hivi hapa nchini yenye jina la Mnyama wa Pori.

Wanatumia kila mbinu na chokochoko kuichafua na kuipuuzisha kama si kuisahalausha kazi NZURI iliyofanywa na WALLACE KARIA katika uongozi wake...

Tuwe wa wazi tu baada ya CHILA TENGA hakuna uongozi wa TFF uliofanya mengi makubwa kwa mpira wa bongo kama sio huu wa KARIA...amefanya kazi kubwa isiyohitaji kubezwa....

Ndio maana kuna genge la wahuni linaloongozwa na huyo bwana mwenye asili ya Mahali ilipotokea ajali ya MV BUKOBA...kuzusha chokochoko yoyote ili mradi LAWAMA na SHINIKIZO liende kwa KARIA kujiuzulu...

Kuhusu hili la GSM, aliyelianzisha na kumshauri CEO wa CLUB hiyo ya MNYAMA aupinge na kuzusha kahoja kepesi ka FAIR COMPETITION ambayo kwa namna yoyote isingekuwa hivyo walivyosema yeye na GENGE lake, ila lengo ni KUHARIBU MCHAKATO MZIMA UTAKAOZISAIDIA VILABU KUJIENDESHA ili ionekane na lawama ziende kwa uongozi kwa kushindwa kuwezesha vilabu vingine vya ligi kuu KUJIENDESHA na kuweza kushiriki vema ligi kuu.

Hasara ni kwa vilabu vingine ukiacha YANGA, SIMBA na AZAM zitaathirika sana mgogoro huu wa kimaslahi ya watu wachache kama huyu BWANA na genge lake.

Kama KARIA asipochukua hatua za haraka kulidhibiti genge hili...basi watakurudisha nyuma na kukuchafua...sio kwa lengo la kujenga, BALI NA WAO WAPATE KUINGIA NAO WALE KEKI YA MPIRA.

Kwenye suala la GSM, ni WAZI kuna masuala ya kimkataba mbali kabisa na suala Simba kutokubali kuvaa nembo ya mdhamini, ambayo hayo ndio yaliyochelewesha PESA kupelekwa kwa vilabu kama walivyokubaliana...na sababu hiyo hiyo ndiyo waliyofanya wajitoe...

Nakaribisha MJADALA...

NJE YA MADA KIDOGO:
Mbona suala la V.A.R tunali COMPLICATE hivi...tufanye kadri ya uwezo...

mbona tukiwa tunaangalia mpira kwa TV inakuwa ni haraka sisi tunaona REPLAY ya matukio ya uwanjani ..hivi haiwezekani kwa AZAM wakatuwekea ka TV ka Inch hata 55" pale uwanjani kanaonesha mechi kwa mwamuzi wa akiba ili amshtue mwenzake wa ndani kama uamuzi wowote labda hakuoona vizuri.

TUFANYE KADIRI YA UWEZO WETU.
[https://res]

MWENYEKITI wa Bodi ya Ligi Kuu Bara, Steven Mnguto, ameibuka na kusema licha ya wadhamini wenza Kampuni ya GSM kutangaza kujiondoa katika udhamini lakini hakuna klabu yoyote iliyolipwa.

Kauli hiyo imekuja ikiwa ni siku moja tangu GSM watangaze kujiondoa kudhamini klabu za ligi ambazo awali waliingia mkataba wa miaka miwili wenye thamani ya Sh 2.1Bil.

Akizungumza na Championi Jumatano, Mnguto alisema kuwa, hilo suala wamepanga kulizungumza hivi karibuni
mara baada ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) watakapokutana.

Mnguto alisema kuwa, wanasubiria wanasheria wao walipitie suala hilo na mwisho wa siku watalitolea ufafanuzi
kwa undani.

“Kiukweli tangu tuliposaini mkataba na GSM nikiri klabu hazijapata chochote. Klabu zimeitangaza GSM kwa muda wa miezi mitatu sasa, kwa hiyo tunasubiri wanasheria walipitie suala hilo tujue tunafanyaje.

“Hata suala la zile nembo kwenye mabega sijui kama zinaweza kutolewa haraka lakini hata hilo litafanyiwa
kazi kisheria,” alisema Mnguto.

Naye Mkurugenzi wa Habari na Masoko wa TFF, Boniface Wambura, akizungumzia hilo alisema: “Sisi
baada ya kupata barua kutoka GSM, suala la mkataba ni Bodi ya Ligi na ni vema akatafutwa Mnguto lakini
kwa upande wa sisi TFF hatuwezi kuzungumzia kila jambo.

“Tayari tumetoa tamko letu jana (juzi) kuhusiana na hilo baada ya kupata barua GSM.” Juzi TFF ilitoa taarifa
kuwa, Februari 7, mwaka huu walipokea barua ya kuvunja mkataba wa udhamini mwenza wa Ligi Kuu Bara
ya NBC kutoka Kampuni ya GSM, hivyo Shirikisho hilo linafanyia kazi barua hiyo na litatoa taarifa kwa wadau.
 
Back
Top Bottom