Wallace Karia: Wanaojiita Wachambuzi sijui wamesomea wapi, hawautendei haki mpira wetu

Ghazwat

JF-Expert Member
Joined
Oct 4, 2015
Posts
23,718
Reaction score
66,267
Rais wa Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania TFF, Wallace Karia kwenye semina iliyofanyika jana, amesema kuwa katika watu ambao hawautendei haki mpira wa Tanzania ni Wachambuzi wa mpira, wanaongea sana mpaka wanatoka nje ya mstari na kuharibu mpira.

"Kuna wanaojiita Wachambuzi, sijui uchambuzi wamesomea wapi. Kusema ukweli katika watu ambao hawautendei haki mpira wetu ni Wachambuzi, wao wanasikilizwa na watu halafu wanatoa maoni yao binafsi".

"Mimi naona wao (wachambuzi) ndiyo wakati mwingine wanaopotosha na kuzua taharuki".

"Wenzetu Wachambuzi au waandishi uliopo hapa (kwenye semina) mkitoka muwe mmebadilika, siyo mechi imeisha unamuuliza Kocha aliyefungwa goli tatu kwamba mwamuzi kachezesha vipi". Amesema Rais wa TFF.
 
Anae simamia Idara ya Michezo pale WASAFI ni mtu wa hovyo sana, yani watangazaji na wachambuzi zote n'gombe tupu kasoro Ambangile, Ricardo na Eddo. Kale kanyakyusa ka JOB JOB ujuaji mwingi content zero kanataka kuongea muda wote
 
Football is the Game of Opinions...,

Hauhitaji kusomea ili kuwa na Opinion, so long as unajua / unapenda mpira basi utakuwa na Uelewa / Opinion...

Kusikilizwa na wengi / wafuasi inamaanisha you are doing something right..., wote wakiwa na mtizamo mmoja basi football would have been boring
 
Tukiachana na wachambuzi hamna mtu wa ovyo kwenye mpira kama walace karia

Ameibeba sana timu fulani hivi kupitia viporo na waamuzi uchwara. Yaani bila ya kupiga kelele, mpaka leo bado ile timu ingekuwa inajimwambafai tu.
 
rais kasema kweli wala si uongo natoa mfano

wingereza

wachambuzi ni wakina

michale owen
beki wa manu ferdinand
tienry henry.

hao ni baadhi ambao wanajulikana kwa sasa lakini toka nyuma mchambyzi wa mpira ukiwa uantizama epl lazima waonyeshe kacheza league mara ngap? kafunga goli ngapi ? na mataji

vilevile huwa wanatabia ya kualika wachambuzi wachezaji kama alan shearer, hata lampard alishawahi pewa air time kusema yake kuhusu mechi kazaaa.
 
Karia ana mapungufu yake.....
Ila TFF yake ndio inaweza ikasimama ikasema imelifanyia chochote soka la Tanzania.
Ni wakati wake Tanzania imeonesha uhai kimpira kidogo.

Anapata lawama Nyingi na chuki nyingi kuliko pongezi, tunaingia mkenge kwenye mtego uliowekwa na wapinzani wake.

Kuhusu wachambuzi nimelia sana Humu, hawana wanachokifahamu zaidi ya Upotoshaji na Ujuaji.
Wachambuzi hawa kwa upotoshaji wao wameifanya TFF iwork under prussure daima.
 
Yeye mwenyewe na mambo ya mpira ni wapi na wapi,aende akaaply uhasibu wake sehemu nyingine na sio kuisimamia hii taasisi hadi ikageuka kuwa Tanzania Football failures.
 
Unaingia mkenge wa maneno ya wapigaji....
" mtu wa mpira".....
TFF mle ndani hawapigi danadana kwamba inahitaji mtu wa mpira.
Ni akili ndio inatakiwa mle.
 
Amekuwa wa hovyo sana na very corrupt...Nikifikiria ule mkataba wa TFF na GSM nashindwa kumuelewa.
Kati ya wachambuzi wa ovyo JF Kwa Sasa ni Ghazwat. Yeye Kila wakati ni kuleta maoni hasi dhidi ya Yanga pekee. Kwake Hakuna kiongozi, mchezaji au shabiki wa Simba anayefanya vibaya.

Ni aina ya mashabiki fuata upepo ambaye Hana msaada wowote Kwa timu anayoshabikia zaidi ya kuipaka mafuta Kwa mgongo wa chupa. Huwezi kumfananisha na Mightier au Gentamycine àmbao nao ni Simba lakini timu, mchezaji au shabiki anapokuwa na udhaifu wanasema ukweli.

Zamani OKWI BOBAN SUNZU alikuwa Bora Sana kiuchambuzi, siku hizi kabebwa na ndugu yake naye kawa wa ajabu!! Bora Scars anaimprove Sana katika uchambuzi, nadhani baada ya kumsema
 
Kumbe kuna wachambuzi wa JF 😂😂😂
 
Rais wa Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania TFF, Wallace Karia kwenye semina iliyofanyika jana, amesema kuwa katika watu ambao hawautendei haki mpira wa Tanzania ni Wachambuzi wa mpira, wanaongea sana mpaka wanatoka nje ya mstari na kuharibu mpira.

"Kuna wanaojiita Wachambuzi, sijui uchambuzi wamesomea wapi. Kusema ukweli katika watu ambao hawautendei haki mpira wetu ni Wachambuzi, wao wanasikilizwa na watu halafu wanatoa maoni yao binafsi".

"Mimi naona wao (wachambuzi) ndiyo wakati mwingine wanaopotosha na kuzua taharuki".

"Wenzetu Wachambuzi au waandishi uliopo hapa (kwenye semina) mkitoka muwe mmebadilika, siyo mechi imeisha unamuuliza Kocha aliyefungwa goli tatu kwamba mwamuzi kachezesha vipi". Amesema Rais wa TFF.
Kwani wewe ulisomea wapi Urais wa TFF?
 
Back
Top Bottom