econonist
JF-Expert Member
- Jul 11, 2015
- 20,189
- 29,663
Shida yako unashindwa kutofautisha upentekoste na cults au wahuni. Unalazimisha wahuni au Cults wawe wapentekoste.Ukristò ni dini ya watu wasomi, wagunduzi, wana sayansi, matabibu, wana anga za juu nk.
Sasa siku za karibuni limeibuka kundi la watu wasiofikiria, wasio hoji, wenye ufinyu wa fikra, wenye kupelekeshwa kibwege kabisa na wahuni wanaojiita mitume na manabii.
Nabii akisema leo kamnyime mumeo unyumba, basi nyumbani siku hiyo mtalala mzungu wa nne.
Nabii akisema kalete mbegu, basi humo ndani hakukaliki lazima mbegu nono ipelekwe kwa nabii.
Walokole wanakonda manabii wananenepa. Kila siku ufukara unawaingia kwa kasi. Wanaangamizwa kwa kukosa maarifa.
Walokole mnatakiwa mbatizwe kwa ubatizo wa moto wa gesi huenda ndipo akili zenu zitafunguka na kuijua kweli ambayo ni neno la Mungu.
Na shida unadhani ulokole umeanza kwa akina Mwamposa. Ulokole au Upentekoste kwa Lugha rasmi umeingia Tanzania mwaka 1928. Na makanisa yalikuwa matanoa tu.
Kanisa la Pentecostal Holliness Association la Paul Derr ambalo baadae liliizaa TAG, pia kanisa la UMPT baadae FPCT la akina Mzee Harris Kapiga, Elim Pentecostal na Kanisa la PAG. Hayo makanisa yalianzisha upentekoste Tanzania kuanzia 1920.
Na ndio makanisa yenye misingi imara ya upentekoste mpaka leo , so achana na wasanii kipimo kiwe makanisa waanzilishi.