kmbwembwe
JF-Expert Member
- Aug 16, 2012
- 10,892
- 7,780
Kwanza serikali ionyeshe hiyo kampuni ya mfalme wa UAE inaingiza serikali kipato gani kama sio kuwahonga vigogo. ni jambo la kustaajabisha kuona wananchi wananyanyaswa na serikali yao kwa manufaa ya wageni. Kwanza hao OBC wanatakiwa kufukuzwa kwani inaelekea wameanzisha koloni ndani ya nchi yetu kwani kinachowapata ndugu zetu wa jamii ya kimaasai ni sawa na kuwa chini ya mamlaka ya kikoloni. chondechonde tusiwapeleke ndugu zetu kuanzisha vita vya ukombozi kutoka na uroho wa viongozi.