Clemence Mwandambo
JF-Expert Member
- Dec 2, 2018
- 1,378
- 1,427
Tanzania mtu kasomea udaktari Kapewa masharti magumu kufungua zahati, alafu mganga wa kienyeji karuhusiwa kutoa huduma hata kwenye banda la nyasi. Kijana tulimsomesha wenyewe kapigwa vikwazo mapaka hapo acha wajazane kwenye umachinga.
Mtu kasomea sheria lakini hawezi kuwa mwanasheria mpaka aende shule ya sheria, kwa mini musiunganishe vyote kuwasaidia vijana? Alafu akiwa wakili wa kujitegemea halipwi na serikali lakini bado tumeweka vikwazo kibao, Dili ni umachinga na bodaboda tu hakuna jinsi.
Mwalimu haruhusiwi kufungua shule, mpaka awe na hekari kadhaa, majengo ya kisasa, vikwazo vya usajili mpaka basi. Waaache wajazane kwenye umachinga na bodaboda, tena tukiwasumbua tutegemee siku moja Yale ya Afrika ya kusini.
Jamani watu wana taaluma zao wako kwenye umachinga, angalieni sheria zinazozuia watu wasijitegemee. Mnazungumza habari za watu kujiajiri lakini mazingira ya watu kujiajiri yamefungwa na wanasiasa. Tatizo wanasiasa hawajuai maisha ya watu, wanaamua kwa kupapasa.