Mleta mada, kilichotokea kwa wajariamali au wamachinga wa kimara kama ulivyosema,hawajabomoa wenyewe bali walibomolewa usiku wa maneno na ndani ya nusu saa hivi zoezi lilikuwa limekamilika.zoezi hili liliendeshwa na kikosi kazi maalumu cha jiji na wakitumia scavator au tingatinga lilokuwa na moja tu ya kuondoa kile kilichoagizwa kufanywa na wahusika.
Katika zoezi hilo,baadhi ya watu wachache sana waliwapa taarifa wenzao ambao baadhi yao waliokoa vitu vyao kulingana na umbali waliokuwepo kufika eneo la tukio lakini zaidi ya 90% ya wajasiriamali hao walipoteza mali zao na kurudishwa kwenye umasikini mwingine.
Katika zoezi hilo, yamesemekana mateja na watu wengine wamefaidika sana ubomoaji huo mfano siku chache zilizopita mtu mmoja aliweka kibanda cha simu ambacho nami nilikiona siku chache zilizopita,ajabu kapoteza kila kitu.kiufupi zoezi hili limewarudisha watu wa hali ya chini katika umasikini wa aina yake.
Wito wangu kwa mamlaka husika, serikali ingewaacha wavuja jasho hao,wanyonge kama wanavyoitwa au wamachinga kama mleta mada alivyosema,wakitafuta mkate wa kila siku kwa mantiki ya kupata pesa ya maandalizi ya kuwapa mahitaji ya msingi ya watoto wanaojiandaa kuingia darasa la kwanza na sekondari na pengine lingeanza mwezi match,2022 ambapo wazazi kama wazazi watakuwa wametimiza mahitaji hayo kwa vijana wao.