Wamachinga Kimara wamehama wenyewe

Utawavumilia hadi lini mkuu...hakuna siku inaunafuu, ni bora watu watii mamlaka wafungur biashara panaporuhusiwa...
Walipewa miezi miwili...wakaongezewa
mmoja....wakaongezewa week mbili.
Kadiri muda unavyozidi kwenda vibanda vinaongezeka..
Mantiki yangu ni wakati gani zoezi hilo lingeweza kufanyika, mfano zoezi lingeweza kufanyika mwakani mwezi march ambapo wazazi watakuwa wameshapeleka watoto wao shule.mbili wangeandaliwa maeneo rafiki ya kwenda badala ya kuwaondoa wasijue pakwenda na hata baadhi ya maeneo yasiyo rafiki walioandaliwa hakuna biashara yoyote inaweza kufanyika na kumpa mtu kipato. Tatu naunga mkono baadhi ya maeneo ambayo hayakuhitaji kusubiri mathalani eneo la posta karibu na chuo cha IFM na ofisi zingine zikiwemo zilizokuwa wizara za serikali, hao machinga au wajasiriamali walicheleweshwa kuondolewa kutokana na mandhari yenyewe ya jiji na historia yake.
Hata hivyo mfano mbezi Louis stendi ndogo ya dala dala na bajaji, eneo hilo kunaweza kujengwa jengo lenye floor moja mzunguko na wajasiriamali wakapangwa vema ground na floor ya moja ya juu, maisha mbona yangeenda.
 
Nyi mnadhani umachinga umeisha!? Subirini 2 years Kam haijaanza kampen nyingine
 
Hili swala la machinga kuachwa hohela kwa kisingizio cha huruma Mimi sikubaliani nalo maana halina uzuri wowote Zaidi ya hasara hasa mbele ya safari ya kipato cha mtu mmoja mmoja kitakacho kuwa endelevu pia naungana na Tundu Lissu sera yake ya kujenga miundo mbinu mizuri ya biashara na kushusha kodi kwa wafanyabiashara Ili kodi zilipike kwa urahisi na hata biashara ndogo zisilemewe na wingi wa kodi kitu kinacholeta hii issue ya wamachinga Ili wakwepe mzigo mkubwa wa kodi na kuleta fujo za kuuza Kila sehemu iliyowazi bila kujali usafi na uwepo wa miundo mbinu wezeshi kwa mahitaji ya mtu anayeshinda sehemu tofauti na anapoishi, kikubwa machinga wa ukweli waombe kupunguziwa kodi kwenye biashara ili biashara zifanyike kwa amani, ila machinga wa uwongo ndo waendelee kupiga kelele za kuachwa hovyo hovyo Ili wawaibie watu na wengine wapate sehemu ya kuzugia mjini na kutapeli watu maana huwezi kudanganya watu unauza sabuni mbili na zinakupa kipato cha kulisha familia na nauli ya kushinda mjini kama siyo mbinu zingine zinatumika hasa utapeli.
 
Machinga wamesharudi maeneo karibu yote jijini. Tatizo la machinga sio dogo kama nchi inavyolichukulia. Mtu anaweza kuvumilia njaa siku 2 tu ya 3 atatpka nje kutafuta chakula hawezi kukubali kufa njaa
Sio kweli kwa hali ilivyokuwa ktk jiji la dar, zoezi hili limefanikiwa kwa asilimia 90, nenda leo mwenge, buguruni, mbagala, gongolamboto kote kweupeee!!!hao walio rudi ni wapi?na maeneo yote yale korofi mgambo wanashinda hapo hadi jioni!!labda kuanzia saa moja usiku ndio kidogo wanapanga panga bidhaa lakini hawana madhara sana, .ki ukweli hadi sasa serikali imefanikiwa sana .
 
Unahisi mwezi march ndo ela zitakua haziitajiki!!!siku hz watu wanalipa ada kwa term..mwezi march hadi april ni malipo ya term ya pili...
Tatizo hili la chingazi na biashara holela likiachwa ...kadiri siku zinavyozidi watu wanazidi kuuziana maeneo..na kusambaa zaidi..so njia sahihi ni kulidhibiti haraka iwezekanavyo...pia ni vyema kufahamu keamba hakuna chinga anayependa kudhibitiwa wengi wanapenda kufanya biashara bila kudaiwa kodi wala ushuru...unaweza kujenga jengo na watu wasikae
 
Hatuwezi kuvumilia ujinga, watu wameombwa waondoke hawakusikia, sasa mnataka Mungu awape nini.
Hatuwezi kua na jiji lililojaa watu wanafanya watakavyo
 
Acha porojo. Watu wanatapeliwa na wavaa suti usiwasingizie machinga.
 
Hatuwezi kuvumilia ujinga, watu wameombwa waondoke hawakusikia, sasa mnataka Mungu awape nini.
Hatuwezi kua na jiji lililojaa watu wanafanya watakavyo
Hamuwezi wewe na nani!?
 
Wawaache bhana Kama wameshindwa kuwatafutia sehemu stahiki, Sasa unamfukuza mtu then humpangii mahali pa kwenda unategemea anaishi vipi?
 
Mkuu@Trubarg, natambua watu wanalipa kwa term sawa lakini huwezi kulinganisha mahitaji ya mwanzo wa mwaka na term zinazofatia. Ieleweke na ikubalike kuwa, siyo kwamba naunga machinga kukaa na kuzagaa holela hapana, tena kuna maeneo kama posta karibu na IFM nilikuwa sikubaliani nao kabisa.mantiki yangu ni kuangalia mazingira tunayoyaendea ya mwanzo mwaka 2022 na watoto wanatakiwa kuwa shule achilia mbali mambo ya kodi n.k.
Nb: ikumbukwe pia ni serikali hii iliyowatunza,kuwafadhili na hata kuwapa mikopo ya vikundi kwa baadhi yao na zaidi vitambulisho vya ujasiriamali au muungwana umeyasahau haya!
 
Hatuwezi kuvumilia ujinga, watu wameombwa waondoke hawakusikia, sasa mnataka Mungu awape nini.
Hatuwezi kua na jiji lililojaa watu wanafanya watakavyo
Mkuu@Telegram, sijakata kuondolewa kwao Lah! Kuhusu muda waliowapa hautoshi hata kidogo, chukulia kama ni ww ungekwenda wapi ukizingatia maeneo tengwa na rafiki ya kibiashara hayapo, maeneo ya wazi wajanja walishajitafunia, leo wanaondolewa ghafla kwa kisingizio cha kuwapa miezi 2au 3 bila kujua waende wapi. Kuwatafutia maeneo ya biashara baada ya kuwaondoa ni kuwaonea wanyonge bure tu.
Ni vema yangejengwa kwanza maeneo husika kisha wapelekwe huko kuliko unyama na uhuni waliofanyiwa ndani ya nchi yao wakati wamelelewa na kulindwa siku zote na hao hao wanaojaribu kubadilika rangi leo utadhani hawakuwepo hapo nyuma.
Viongozi wa nchi hii ni kushindwa kuwajibika kwa kusimamia kile wanachokiamini hasa pale wanaposhindwa kuelewana na boss wake,ni kansa inayolitafuna taifa.
 
Mkuu hiyo 20k three years ago bado ipo tu..
 
Uzuri walitangaziwa kuondoka kabla hawavunjiwa,kwahiyo kosa ni la kwao hao machinga,hawasikii wanafikiri ni mzaa
 
Kiukweli ndugu zetu wameumizwa pakubwa sana na ukizingatia tunakwenda nyakati mbaya za watu kupeleka watoto shule zetu za wanyonge na matokeo yake ndo hivi.busara zingetumika kuwavumilia kwa muda tu.
Mnajua kusingizia kupeleka watoto shule wakati hata hayo majukumu hauyatimizi. Elimu ni bure siku hizi.
 
Machinga wamesharudi maeneo karibu yote jijini. Tatizo la machinga sio dogo kama nchi inavyolichukulia. Mtu anaweza kuvumilia njaa siku 2 tu ya 3 atatpka nje kutafuta chakula hawezi kukubali kufa njaa
Si kuna mkuu fulani wa mkoa alisema wakirudi anaachia ngazi? Kama amesahau maneno yake haya, mkumbusheni kuwa draft ya barua ya kujiuzulu imeishawekwa mezani.
 
Si kuna mkuu fulani wa mkoa alisema wakirudi anaachia ngazi? Kama amesahau maneno yake haya, mkumbusheni kuwa draft ya barua ya kujiuzulu imeishawekwa mezani.
Usiwaamini wanasiasa hata kama akikwambia kitu cha kweli usimwamini kwanza
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…