Makelele ya kwamba wanaonewa sio kweli, serikali ipo makini sana na inajua inachokifanya na kwa faida yao hao wanaojulikana kama wamachinga.
Ukweli mchungu na unauma, wafanya biashara hawa kwanza ni wakwepa tozo wakubwa, japo wana vibali lukuki, vingi ni feki na wanapobanwa hutoa chochote ili wawe huru.
Haiwezekani nimekodi mlango au fremu ya duka nimefungua duka ninalipa tozo za aina yote na mashine za VAT ninazo kwa maana nipo katika eneo ninalolipia kuanzia kwa mwenye jengo hadi serikalini, muda si muda mbele ya duka zetu wanakuja hawa wamachinga na kuweka biashara zao mbele ya duka langu na wanauza bidhaa zilezile ninazoweka mimi dukani, na zaidi hujazana kwenye barabara na kuweka na kuonekana kama wapo kwenye maandamano, hadi barabara inakuwa haionekani, wanasababisha ajali za kila siku.
Serikali imefanya vyema kuwaondoa watu hawa katikati ya miji, mbona sehemu au Tanzania ni kubwa na inasehemu nyingi tu zilizo wazi, tatizo la wao kuwekwa na kufanya biashara zao ni nini? Kama ni wateja mbo kizuri chajiuza? Wateja watawafuata huko huko waliko na kutajaa, hivi hawajiamini?
Haiwezekani nyote mkarundikana sehemu moja kama wale ndege wa baharini, halafu ukizingatia wateja si wote wanakaa ndani ya jiji wengi wao ni kutoka katika vitongoji vya nje au kandokando ya mji, kuna haja hata magereji ya magari yakaondolewa ndani ya mji na kutengewa sehemu nje ya jiji.
Na jiji la Dar ni kubwa ile sehemu ya jangwani inaweza kuboreshwa na kuwatandaza wamachinga kuanzia baharini hadi mujini, ikiwezekana Hospitali kuu ya Muhimbili inatolewa au kuhamishwa nje ya jiji na kuwekwa kwenye sehemu kubwa kuliko ilivyo sasa.
Watu wapanga miji hio sehemu iliyondani ya red inahitaji kuboreshwa katika kiwango cha kimataifa na itaweza kubeba wamachinga wa kila aina.