Wamagharibi kumbe kweli walikubaliana na Urusi kutoongeza Wanachama wa NATO kuelekea Mashariki, gazeti laibua ushahidi

Mkataba upo, we ingia mitandaoni uchungulie! Urusi sio mpuuzi, kiasi kwamba alete madai ambayo hayajaandikwa popote. Mkutano wa Macron na Putin, Macron alikumbushwa makubaliano ya mwaka 1991 kati ya Urusi na nchi za Ulaya Magharibi, kutoongeza wanachama wa NATO kutoka nchi za iliyokuwa Umoja wa Soviet
 
Mbona tunajisahaulisha chanzo cha Cold War kilikuwa nini. Wasovieti walipopeleka makombora ya nyuklia pale Cuba Marekani ilicharuka ikatuma meli za kivita, ikaweka naval blockade kwa Cuba na ikatoa demand makombora yaondolewe. Wakati huohuo Marekani ina makombora Ulaya Mashariki, ikabidi pande zote mbili ziyaondoe.

Sababu za vita ya Georgia ni kama hizi za Ukraine. Kilichotokea Georgia ni Southern Ossetia na Abkhazia na kilichotokea Ukraine ni separatists wa Donbass region. Ukraine hana sababu ya kuwafia NATO na Marekani, aachane na mpango wa kujiunga nao maana ndio hivyo miaka 8 ana vita na msaada hautoshelezi. Mbona Finland inapakana na Urusi na iko peaceful miaka yote tangu Cold war, tena hiyo iliwahi vamiwa na USSR kwenye WW2
 
Achana nae huyo huwa anabishana na radio
 
Hakuna makubaliano hayo, hicho ulichokopi siyo makubalian. Niliwahi kuleta hapa transcripts zinazoonyesha jinsi ambavyo Yelstin alivyokuwa anamuomba Clinton atamke kuwa NATO haitapanuka kwa sababu alikuwa anataka kuwapooza warusi waliokuwa wanaogopa NATO, lakini hakukubaliwa. Soma maongezi yao yote kwenye transcripts hizi.

Ukweli unaomsumbua Putin nia huu uliotamkwa kwa makini na na huyu mama wa kihindi

 

Attachments

Jf ni kijiwe cha uwongona uwongo huo unapendwa sana kwasababu unafurahisha mioyo ya wengi.
 
Mkataba upo wapi?

Sihitaji kwenda mitandaoni kuchungulia. Anayesema mkataba upo auweke hapa na tarehe ambayo mkataba huo ulisainiwa. Mbona mikataba mingine kati ya Marekani/nchi za magharibi na Urusi inafahamika hadharani? Huo mkataba mmoja tu uko wapi?

Urusi imeibua madai ambayo hayapo kimkataba! Kama mkataba upo, ungekwisha wekwa hadharani kama uthibitisho na sio kusema tu kwamba wamekubaliana. Hayo madai yameandikwa wapi kimkataba?
 
Kasome " The Minsk Agreement II". Kuna details humo za kuondoa vita kati ya Ukraine na Urusi
 
Kasome " The Minsk Agreement II". Kuna details humo za kuondoa vita kati ya Ukraine na Urusi
Hayo ni makubaliano ya kumaliza mapigano yaliyopo tangu mwaka 2014 mashariki mwa Ukraine. Hayo sio makubaliano kuhusu NATO kutopaswa kuongeza wanachama kuelekea mashariki mwa Ulaya.

Nilichohitaji ni mkataba kati ya NATO na Urusi unaohusu NATO kutopaswa kuongeza wanachama katika jumuiya hiyo kutoka katika mataifa ya Ulaya Mashariki hasa mataifa yaliyokuwa miongoni mwa USSR.
 
Kasome " The Minsk Agreement II". Kuna details humo za kuondoa vita kati ya Ukraine na Urusi
wewe unazungumza maongezi ya mwaka 2015 baada ya Urusi kuvamia crimea. Tafuta historia kamili baada ya USSR kuvunjika na jinsi Ukraine ilivyokubali kuwapa urusi silaha zake za Nuklia
 
Hakuna makubaliano kama hayo, ni uongo mtupu.
 
wewe unazungumza maongezi ya mwaka 2015 baada ya Urusi kuvamia crimea. Tafuta historia kamili baada ya USSR kuvunjika na jinsi Ukraine ilivyokubali kuwapa urusi silaha zake za Nuklia
Urusi akarithi mali zote za iliyokuwa USSR zikiwemo balozi,na madeni yote . Ukraine akataka kuwe na mgawanyo.
 
Mwanzo sikujua ila baadae nimejua kumbe Russia ni mpinzani wa Jamii za kishetani, vita hii ataumia sana lakini mwishoni kabisa atashinda na ndipo ataanzisha uamsho.
 
Mbona kuna mabaunsa wanatembea na mke wako mwenye cheti cha ndoa na hujawafanya chochote?
Mtafute mke wa mtu tembea naye kisha mwenye akukute halafu umwambie hana cheti cha ndoa uone kama utabaki na marinda.
 
Urusi akarithi mali zote za iliyokuwa USSR zikiwemo balozi,na madeni yote . Ukraine akataka kuwe na mgawanyo.
Siyo kweli; soma historia . Kila republic ilirithi mali na madeni yaliyokuwa kwenye ardhi yake. Ukraine ilirithi silaha nyingi sana za Nuclear, lakini ikazikataa, ndipo zikachukuliwa na Urusi. Vile vile Ukraine ilirithi jeshi kubwa sana isipokuwa baadhi ya wanajeshi wakaamua kujiondoa na kurudi urusi. Kazakhstan ilirithi maroketi ya kwenda anga za juu, ingawa urusi imekuwa bado inayatumiwa kwa kuwalipa. Balozi ziligawanywa kulingana na ni Bbalozi aliyekuwapo wakati huo. Kwa mfano, iwapo Barozi wa Urusi Tanzania alikuwa anatoka Belarus, basi Balarus ndio waliobaki na ubalozi huo, japo kwa makubalino waliewaza pia kubadilishana na republic nyingine. Kwa hiyo balozi zote zilizochukuliwa na urusi ilikuwa ni kwa makubaliano na republic husika.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…