Wamakonde wa Kipumbwi na Mapinduzi ya Zanzibar 1964

Wamakonde wa Kipumbwi na Mapinduzi ya Zanzibar 1964

Umedadavua vizuri sana; shukran. Mambo mawili. Mosi, inatoa picha Sultan Seyyid Said hakuwa mzalendo nchi yake ya Oman. Haikupata kusikika ufalme kuhamisha kitovu cha utawala kwenda ardhi nyingine ya mbali; sio himaya ya Roma, Uajemi, Ujapan, Uingereza, n.k ziliwahi kufanya hivyo. Something was wrong.

Pili, kama mojawapo wa watoto aligawiwa Zanzibar na kwa sehemu kubwa kizazi cha Zanzibar kilikuwa na nasaba ya Oman hisia za "huyu sio mwenzetu" hadi kupelekea mapinduzi zilitokea wapi?
Mapinduzi ya Zanzibar hayakulenga kumuondoa Sultan, hakuwa the main Target, Mapinduzi ya Zanzibar yalikuwa ni kwa ajili ya chama cha ZNP. hizo story za Sultan na propaganda uchwara za CCM kujaribu ku justify walioyafanya.

walichokifanya ni kutengeneza Picha kama vile Sultan alikuwa ni mkoloni wao wamepindua wakoloni kitu ambacho ni PUMBA
 
nahivyo ndivo ilivyokuwa. na ndio Mana Wa Oman walikuwa wanazamia Zanzibar kuja kusaka life na sio wazanzibari kuhamia Oman kwenda kusaka life
I now get the point kwanini baadhi ya wanasiasa wanaiita Zanzibar kama Dola la Zanzibar. Kumbe imewahi kuwa mwamba!
 
Hao viongozi wa Zanzibar waliokubaliana na Oman kuwaondosha wareno ni akina na nani na mwaka gani

Zanzibar kabla ya kutawaliwa na Ureno walikuwa wakitawaliwa na wafalme wa kishirazi, jaribu kutafuta historia ya Kilwa Empire utapata habari zao, hao jamaa walikuwa na kama area Commissioners wao au kwa sasa tunaweza kuita wakuu wa mikoa kila maeneo. kule Unguja walikuwa wanaitwa Winyi wakuu. Baada ya Ureni kuchukuwa utawala wale wafalme wakapotea, ila hawa area commisioners waliendelea kukuepo kienyeji na ndio walioshiriki hili zoezi.
 
Waliwezaje kuji-organise wakati kila mwinyi mkuu alikuwa na utawala wake
 
Waliwezaje kuji-organise wakati kila mwinyi mkuu alikuwa na utawala wake

mkuu vitabu vipo jaribu kutafuta usome, zililwenda deligation kadhaa kule oman, Na barua ya mwanzo kutumwa nahisi mpaka leo ipo katika makumbusho.

kuji organize kwao haikuwa jambo gumu mana walikuwa ni watu wanaoelewana vizuri, ni tofauti na machifu wa Bara mana walikuwa hawanafanani kabisa.
 
Sasa ikawaje baada ya wao kuwafukuza wareno wakatawala wao
 
dudus

Hio ishu ilikuwa i hivi.

Sultana wa Oman aliingia mkataba na viongozi wa Zanzibar na ukanda wa pwani kiujumla kuwa akiwezo kupambana na Mreno akamng'oa wao watakubali kuwa chini ya himaya yake. Sultan alipambana na mreno mpaka akamfurusha kabisa akabakia Msumbuji huko ila hapa kwetu akakimbia, ndio Sultan wa Oman alipoanza kuwa mtawala wa Zanzibar. na baadae alihamisha makao makuu yake kuwa Zanziba kwa maana Zanzibar ilifikia kuwa nahadhi kubwa zaidi kwa kila kitu kuliko Oman. Ila Baada ya Sultan Sayyid Said kufariki kulitokea ugomvi mkubwa baina ya watoto wake katia nani atarithi ufalme ule, Na ndio serikali ya uingereza iliingilia kati na ndio wakazigawa nchi na Oman ikawa kwake Mbali Na Zanzibar ikawa kwake mbali, kwa hiyo kila sehemu pakaanzishwa utawala wake ambao hapakau na maingiliano yoyote baina yao. Na ndio. Kwahiyo Masultan wa Zanzibar walikuwa na asili tu ya Oman kifamilia lakini hapakuwa na maingiliano baina ya Zanzibar na Oman.

Na ndio mana baada ya mapinduzi Sultan alikimbilia U.K na ameishi maisha yake yote kama ni mkimbizi kutoka Zanzibar na sio mu oman, mana hajawahi kuwa mu oman alikuwa ni Mzanzibari.
Umetoa historia ya kweli hivi ndio inavyotakiwa watu wasome wasiwe wabishi tu au kuburuzwa
 
Historia inayofundishwa mashuleni kwamba Sultan alihamisha makao yake kutoka Muscat hadi Zanzibar huwa siielewi!

Kwamba wakati Sultan yuko Zanzibar anatawala kiti cha Muscat hakikuwa na mtu bali order ilitokea Zanzibar? Kama ndio hivyo, ina maana wakati mapinduzi yanatokea still kiti cha Muscat bado ni kitupu?

If so, mbona historia inayofundishwa Oman haioneshi kiti cha Muscat kuwahi kubaki kitupu? Maana hata Jamshid alipokimbilia London na kuishi almost maisha yake yote huko, usultan wa Oman uliendelea! Somewhere tunapigwa changa la macho!

Kaneno kalikotumika kwenye hiko kitabu cha historia ninayoizungumzia kuhusu kuhama kwa Sultan ni "Shifted".
Nafikiri Masultan walikuwa wengi, siyo Seyyid Said pekee...so alivyokuja Zenji kule Muscat kulikuwa na mwingine
 
Nafikiri Masultan walikuwa wengi, siyo Seyyid Said pekee...so alivyokuja Zenji kule Muscat kulikuwa na mwingine
Kimsingi sultan ni mfalme; hapawezi kuwa na wafalme zaidi ya mmoja katika himaya moja kwa wakati mmoja.
 
Inside10,
Nashangaa kuwa huijui historia ya Waomani kuja Zanzibar.
Waomani waliitwa na Wazanzibari.
Kikao hicho au kura hizo..
Wazanzibar waliamuaje kwa umoja wao kwamba waOMAN waje?!
In short mechanism gani ilitumika kupata maoni ya wazinzabar ?
 
Mtazunguka weeeh lakini ukweli ni huu,

Hapakuwa na cha makubaliano baina ya wazawa wala babu yake na wazawa wa eneo la Zanzibar kuhusu Waarabu kuja kumuondoa mkoloni

Ni biashara ambayo ndio ilifanya waarabu tofauti tofauti (na siowaoman pekee) kufika Zenji na maeneo mengine ya Afrika kama vituo kuelekea maeneo tofauti kusaka mahitaji yao

Kadri muda ulivyoenda baadhi walilowea, na hata mreno alipofika sio kama hakukuta waarabu waliokuwa wanaishi kule

Na ndio waliomba msaada kwa waarabu wenzie na ndipo sultan akajiongeza na kuleta raia hatimae kuwafurusha wareno

Biashara ilivyonoga na utumwa kushika kasi ndipo sultani alipoona ahamishie kabisa makazi yake na watumishi mbalimbali ili aendeleze ufalme wake

Na ndicho kilichotokea;

Ukiniambia hao mamwinyi weusi kutawala Zanzibar sio kweli
 
walichokifanya ni kutengeneza Picha kama vile Sultan alikuwa ni mkoloni wao wamepindua wakoloni kitu ambacho ni PUMBA
Hivi mtu atome Asia huko aje tawala zanzibar huo sio ukoloni?!
Nasema hivi yaheshimiwe mapainduzi matukufu ya Zanzibar
 
Kikao hicho au kura hizo..
Wazanzibar waliamuaje kwa umoja wao kwamba waOMAN waje?!
In short mechanism gani ilitumika kupata maoni ya wazinzabar ?
Inside10,
Sina taarifa za "mechanism."
Kilicho katika historia ni kuwa Waomani baada ya kuitwa walikuja wakapigana na Wareno na kuwatoa Zanzibar.
 
Back
Top Bottom