Ugomvi wa Trump na Bolton ni kwa sababu Bolton alikuwa anamuona Trump ni kiazi asiyeelewa kitu chochote kuhusu foreign policy na diplomasia, kama vile alivyoamka tu akataka picha za kuuza sura na Kim Jong Kiduku huku hakuna hata mtu mmoja kwenye baraza lake la usalama wa Taifa anayeelewa huko kukutana kwao kutafanikisha nini.
Then Bolton warmonger akapigwa chini. Baada ya hapo hatukumuona Marekani akivamia ardhi ya yeyote. Tukaona Marekani anapunguza unnecessary military presence in foreign soils kama kuondoa majeshi Afghanistan. Tukamuona Marekani anaendeleza dialogues badala ya kutumia nguvu tu, ndio huko ziara na Kim Jong.
Hao kina Bolton na foreign policy zao wasingeweza shauri hivyo. Badala yake wao ni milipuko na umwagaji damu tu. Sasa unamuitaje Trump kiazi, kisa hajaua bila sababu?
Trump akuwahi kukumbana na Arab Spring kama Obama au mashambulizi ya September 11 kama Bush kwa hiyo hatujui ange react vipi kama angekutana na changamoto kubwa kama hizo,
Kwahiyo Obama kwa kutumia ushauri wa kina Hilary Clinton alikuwa na akili sana kuivamia Libya kisa Arab spring, ila Trump ni kiazi kukutana na wakuu wa nchi nyinginezo wazungumze?
Okay tuseme Obama hakujua namna ya kureact dhidi ya Arab spring akaishambulia Libya mwaka 2011 (na tusimuite kiazi).
Mpaka Obama anaondoka mwaka 2017 miaka 6 yote alifanya nini kuleta hiyo demokrasia walioisema Libya?
Kilaza nani hapo sasa.
Bado Obama kwenye kuishambulia Syria wamezalisha wakimbizi wa Kiarabu mamilioni, ambao wameharibu utamaduni wa nchi na miji ya kizungu. Kuna migrant crisis inaendelea Ulaya, Ulaya hii ambayo ni mshirika mzuri wa kibiashara wa Marekani hivyo Ulaya akifeli na Marekani anapata hasara.
Bush alidai kwamba Iraq kuna magaidi na silaha za maangamizi, na hakuzikuta hata debe moja. Kaipiga Iraq 2003 mpaka leo haijatengamaa iko prone na ISIS, kuna factions za Sunni na Shia. Marekani baada ya kukosa ilichodai lakini bado haikuleta amani iliyoikuta Iraq.
Bado unaona kilaza ni Trump?
Changamoto mojawapo kubwa Trump aliyokutana nayo ni COVID-19 ambayo alifeli vibaya sana kui handle mpaka kupelekea kupoteza urais.
Alifeli vipi dhidi ya COVID-19, haikuenea kwa uzembe wa Trump hata angekuwa Rais nani bado ingeenea. Hakuna Rais angeua virusi kimiujiza. Ila failure ya Marekani kuvamia Iraq kwa visingizo vya silaha za maangamizi ni ya wazi, failure ya kuivamia Libya eti kuleta demokrasia na badala yake kuiharibu ni ya wazi.
Trump angefeli yeye kama yeye kwenye COVID hawa Democrats wangeitumia kama agenda ya kampeni but no one buys this, Trump is leading kwenye maoni.
Pia Trump hakuondoa majeshi ya US Afghanistan aliyeondoa majeshi ni Biden tena baada ya kukuta makubaliano mabovu yaliyokuwisha kufanyika kati ya Trump na Taliban.
Majeshi hayaondolewi kama magunia ya mapera, hata uhuru haukuwa wakoloni wanafyatuka usingizini leo kesho wanaondoka. Majeshi yanaondolewa gradually na aliyesaini kuyaondoa ni Trump, Biden alimalizia utekelezaji na kuenda kwenye misingi ya Trump.
"... The Trump administration in February 2020 negotiated a
withdrawal agreement with the Taliban that
excluded the Afghan government, freed 5,000 imprisoned Taliban soldiers and set a date certain of May 1, 2021, for the final withdrawal."
Alafu Trump alitaka kuzuia wahamiaji haramu, ambapo Biden na Kamala wanaruhusu shamba la bibi. Pia Trump anataka kufufua manufacturing ya Marekani, hao Democrats wao wamegeuka wachuuzi wa bidhaa za Kichina.
Trump anamzidi mbali akili Biden na Kamala wake, Obama anamzidi mbali failures Trump. Bush huyo hadi anastahili kuwa prosecuted kama hao majenerali wa Nazi Germany.