Ndengaso
JF-Expert Member
- Jul 18, 2014
- 7,831
- 14,259
Kupitia Ukurasa wa Instagram, Ikulu ya Marekani ilipost picha ya Rais wa Marekani akiwa pamoja na Mwenyeji wake Rais wa Ukraine, baada ya kufanya ziara ya kushtukiza na iliyokuwa ya siri kubwa mpaka kufika, picha hii ilifuatiwa na maneno kwamba Ukraine bado ipo Imara na hakuna wakuizuia Marekani kusimama na Ukraine (Tafsiri isiyo rasmi)
Hata Hivyo, maoni ya Wananchi wa Marekani hayakubaliani na msimamo wa Ikulu ya Marekani; Maoni yalioongoza yakiwa na ujumbe usemao, Serikali iache kupoteza fedha za walipa kodi na hicho inachofanywa itasababisha Vita ya Tatu ya Dunia.
Maoni mengine yalisema tumechoka na utawala huu kutuma fedha zetu tulizozipata kwa shida kwenda Ukraine; Jenga Marekani kwanza (Akimaanisha sera ya Raisi aliopita Trump, yakuijenga America kwanza).
Mwingine akilalamika Rais kushindwa kutembelea Ohio kufuatia Janga la kumwagika kwa kemikali ambalo limesababisha Raia zaidi ya 5000 kuhamishwa na vifo vya wanyama zaidi ya 3000.
Ikumbukwe uvaamizi wa Urusi nchini Ukraine unatimiza mwaka mmoja sasa na Marekani imekuwa ikiongoza mapambano ya kuipinga Urusi ikiwemo kuiwekea vikwazo mbalimbali vya kiuchumi vikwazo ambavyo sio tu vimeyumbisha uchumi wa Urusi bali Dunia nzima kutokana na kupanda kwa gharama za nishati na nafaka ambavyo asilimia kubwa vilikua vinatoka Urusi na Ukraine.
Ni yapi Maoni yako ?