Chifu mkuu
JF-Expert Member
- Jan 6, 2025
- 422
- 489
Viongozi wa jamii wa kimasai Malaigwanani Zaidi ya sabini katika wilaya ya Monduli Mkoani Arusha wametoka tamko la kukipongeza chama cha Mapinduzi CCM kwa kumpitisha Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kuwa mgombea urais mwaka 2025, Dkt Balozi Emmanuel Nchimbi kuwa Mgombea Mwenza Pamoja na kumpata Makamu mwenyekiti wa chama hicho Steven Wasira.
Viongozi hao wakizungumza katika mkutano wa hadhara wilayani monduli katika kijiji cha Nanja mbele ya Mbunge wa jimbo la Mondulu Fredrick Lowassa wakati wakizungumzia mgogoro wametoa pongezi hizo huku mbunge huyo akiungana na tamko hilo.
Pia soma: Pre GE2025 - Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025
Pamoja na hili wamepinga juhudi za kudai fidia katika eneo lililokuwa na mgogoro kwa kusema kwamba maazimio yaliyowekwa na marehemu Edward Sokoine, ambaye alikuwa Waziri Mkuu wa Tanzania, yanaweka wazi kwamba eneo hilo linapaswa kubaki kwa madhumuni ya malisho na mazoezi ya kijeshi, na hivyo hayapaswi kutumika kwa manufaa binafsi.
Aidha walisisitiza kuwa tamko la kikao cha Malaigwanani halitaki fidia na litasimamiwa ili kuepuka matumizi mengine ya eneo hilo.
Mbunge wa Jimbo la Monduli, Fredrick Lowassa, amesisitiza kuwa eneo hilo linatumika kwa mafunzo ya kijeshi, na uwepo wa taasisi za kijeshi za kimataifa katika Monduli kunaleta heshima na mahusiano ya kimataifa kwa jamii na nchi nzima