Wamasai wameanza kuogopeka jijini Dar es salaam

Wamasai wameanza kuogopeka jijini Dar es salaam

Kufuatia tukio liliofanywa na member wa umasaini la kifo cha aliyekuwa mkurugenzi wa kiwanda cha kuchakata unga wa makopo ya plastiki, baadhi ya watu wanapata hofu wanapomuona mtu akiwa kwenye vazi la shuka, hususan kobeto likiwa linaning'inia pembezoni mwa kiuno

Twende kwenye tukio halisi, mida ya saa kumi jioni nilivuta chombo kimoja cha kinyaturu na kukitupia gesti kwa ajili ya mashambulizi, nikiwa kwenye kioski cha chips umbali wa mita kadhaa kutoka hapo nikashangaa simu inaingia, binti akinitaka niwahi haraka kuna jambo haliko sawa

Nikiwa nawahi eneo la tukio, nikakutana na mwamba anatoka kibati akiwa amevaa vesti na kujifunga taulo. Baada ya kuingia ndani ya fensi nikakutana na jopo la wamasai wakiwa wamesimama na mhudumu wa gesti hiyo, nikaskia "Kwa hiyo hatuwesi pata chumba". "Ndiiioooo, mtaniwia radhi" kwa sauti ya kutetemeka, "Basi tutalala hapa mapokesi", "Hapana kaka zangu, boss atagomba", basi wakawa wameondoka, mhudumu akavuta pumzi kubwa sana na kuingia maliwatoni kulimwaga kojo. Baada ya kuingia room nikamkuta shemeji yenu akitetemeka eti kuna wamasai wapo hapo nje

Dah! Na hili nalo mkalituzame kwa kweli
Mnawaonea bure. Nao, ni binadamu kama wengine
 
Boss mzima una kiwanda kikubwa unashindwa kuwa na "BOMBA" aka MGUU WA KUKU? Hao wamasai na mapanga yao kama angekuwa na "MKWAJU" aka GITAA wasingemsogelea maana angewafumia UBONGO kabla ya kumfikia.
 
Boss mzima una kiwanda kikubwa unashindwa kuwa na "BOMBA" aka MGUU WA KUKU? Hao wamasai na mapanga yao kama angekuwa na "MKWAJU" aka GITAA wasingemsogelea maana angewafumia UBONGO kabla ya kumfikia.
Zamani kwa dar wamasai
Walikuwa na gathering zao
Mahakama zao,walikuwa wanakutana hapo wana address matatizo yao wenyewe na walikuwa wana shugulikiana kama mtu kafanya kosa anadhibiwa pale
Na kupitia hapo wengi walikuwa wanatambuana
Now days utakuta mtu anajifanya kuvaa shuka sijui lubega anajifanya mmasai
Kumbe wengine siyo

Ova
 
Hakuna kiumbe muoga kukamatwa na police kama masai.... yupo radhi akimbie ajiokoe, aache mali zake hata mke
Kweli mkuu kuna Masai alikua anafanya kazi ya Ulinzi kwa Mzungu kule Zanzibar sasa aliiba Milioni ishirini kwenye kutoroka akakamatwa na polisi, Yule polisi akamwambia Masai lete hizo peza zote na wewe ondoka kapande boti ukimbie nimekusamee Masai akafurahi akaondoka mbio yule polisi akazichukua zile milioni Ishirini.
 
Back
Top Bottom