Wamasai watakaochelewa kuhamia Handeni, kitakachowapata hawataamini

Ardhi yetu iko wapi? Ardhi mali ya serikali.

Profesa Shivji ameeleza vizuri kuhusu ardhi ni mali ya nani, na ni hatua gani zichukuliwe pindi serikali ikitaka kuichukua, na sio kupiga wananchi na kuwahamisha kwa shuruti. Bila machafuko kutokea nchini na kupeana adabu, sheria za nchi hii zitaendelea kufuatwa kwa utashi wa rais na genge lake.
 
Makubaliano yatapatikana tuu hata kwa virungu na mtutu wa bunduki. Dola ina nguvu sana.

Kwa hiyo kwasasa wananchi sio wenye nguvu tena bali dola. Uko sahihi maana serikali hii haiko madarakani kwa ridhaa ya wananchi bali nguvu ya dola.
 
"Kitakacowapata hawataamini" kumbe mnakiri bado tupo kwenye utawala wa kidikteta.

Hao wanaohama waachwe wahame, wasiohama wasisumbuliwe, lakini sio kulazimisha kutoa ardhi yetu kwa mjomba tena kwa mabavu huku chawa mkishangilia.
Sisi tunasubiri nyama za ng'ombe wa wakaidi
 
Sheria zimeandikwa vague kwa makusudi. Ndiyo maana kila mtu anatafsiri yake. Naibu waziri anatafsiri yake, Shivji anatafsiri yake. Lakini mwisho wa siku, serikali inahamisha inayetaka kuhamisha. Mambo hayo yalianza tangu enzi za Nyerere, huyo Shivji si alikuwepo?
 
Kwa hiyo kwasasa wananchi sio wenye nguvu tena bali dola. Uko sahihi maana serikali hii haiko madarakani kwa ridhaa ya wananchi bali nguvu ya dola.

Siyo kwa sasa tuu. Tangu nchi ipate uhuru watu wanahamishwa. Mfumo ni ule ule na umebaki mpaka leo.
 
Waache waendelee kudanganywa na Wakenya walio mabingwa wa kuswaga Wamasai nje ya conservation areas bila fidia kama Mau forest!
 
Umeongea ukweli kabisa, mfano ile operesheni tokomeza ujangili kipindi cha Jk iliacha makovu mengi na kashfa nyingi chafu, hii watawadhibiti na kudeal nao kimya kimya
 
"Kitakacowapata hawataamini" kumbe mnakiri bado tupo kwenye utawala wa kidikteta.

Hao wanaohama waachwe wahame, wasiohama wasisumbuliwe, lakini sio kulazimisha kutoa ardhi yetu kwa mjomba tena kwa mabavu huku chawa mkishangilia.
Sio kubembeleza kila kitu
 
Zinatumika sana tuu. Labda wewe ni mgeni nchi hii. Kila uchaguzi dola inamwaga damu Zanzibar. Mbona hushangai?
Una ushahidi wa unachokisema? Kwa hiyo mnataka kumwaga damu ya wamasai kule Loliondo ili nafsi za Wazenji zifurahi?
 
Una ushahidi wa unachokisema? Kwa hiyo mnataka kumwaga damu ya wamasai kule Loliondo ili nafsi za Wazenji zifurahi?

Kama unaishi Tanzania usingeuliza huo ushahidi. Lakini ngoja nikusaidie hapa

Wamasai sio Jamii ya kwanza kuhamishwa. Watu Kila siku wanahamishwa kwa sababu mbali mbali from ujenzi wa miundombinu, maeneo ya jeshi, hifadhi nk

Hawa mayeroo watahama tu kwa hiyari au shurti kama wanajiona wao ni special sana watakipata wanachokitafuta.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…