Wamejaribu kutusahaulisha Bandari zetu lakini wapi!

Wamejaribu kutusahaulisha Bandari zetu lakini wapi!

Ngongo

Platinum Member
Joined
Sep 20, 2008
Posts
20,654
Reaction score
35,887
Heshima sana wanajamvi,

Tangu sakata la kuuzwa Bandari za Tanganyika tumeshuhudia maigizo,vibweka na Mbwembwe zikifanyika nia na madhumuni ni kutusahaulisha juu ya kuuzwa Bandari zetu kwa waarabu wa hukoooo Dubai UAE.

Walianza na karata ya kununua magoli kabla hatujakaa sana wakatuletea ujanja wa kuunda wizara mpya ya DP World na kumpachika uwaziri yule Prof alikimbia huko Singida.

Prof Uchwara kapachikwa pale kutupooza waTanganyika na machungu ya Bandari zetu kuuzwa na waZanzibar.Hili nalo limeshindwa kupooza moto wa Bandari za Tanganyika.

Wakubwa baada ya kubaini bado wa Tanganyika wana uchungu na Bandari zao wakaamua kuja na mkakati wa kuingiza UDINI.Hili walifanikiwa kuwasomba watanganyika wajinga wajinga kama The Boss ,FaizaFoxy ,The Big Show ......Hawa ukichanganya na Masheikh ubwabwa hawajui thamani ya urithi wa waTanganyika wameweka mbele udini kuliko kutazama uhalisia.

Viongozi baada ya kubaini waTanganyika bado ni wamoja wakaanzisha mchakato mwingine wa kututoa kwenye reli HAKI JINAI.WaTanganyika bado tunadai BANDARI zetu.
 
Mbona mnajisitukia nyie vibaraka?!!! Maisha yamekua yakienda siku zote mbona?!!! Kuna muda wowote umepita bila kuwa na tukio lolote?!! Kwahiyo kila kitu kisimame kwa vile nyie vinabo mnataka kutwerk hapo viwanjani?!!


Halafu mngejua watu wala hawawafikiriii, wapo na mambo yao tu ya kujenga taifa hili......hamtomtisha yoyote na hamtoweza!!
 
"watanganyika wajinga wajinga kama FaizaFoxy"

Hii nimeipenda mkuu Huyu bibi nitamnyoosha.
 
Huku mkoani mtaani kwetu hata hawajui kuwa kesho ni yanga dei nimeshangaa Sana, kweli bandali imetrendi.
 
Issue ya bandari imekataa kuwatoka watanganyika kabisa, hua wanadai ni watu wamatukio lakini hilo naona wamegoma kabisa maana mijadala ni mikubwa sana , halafu kuwakamata watu wanaoujadili ndio wanaharibu zaidi watu wanaona mmeleta mkataba wa hovyo na bado mnatumia nguvu kutuumiza hapana
 
Issue ya bandari imekataa kuwatoka watanganyika kabisa, hua wanadai ni watu wamatukio lakini hilo naona wamegoma kabisa maana mijadala ni mikubwa sana , halafu kuwakamata watu wanaoujadili ndio wanaharibu zaidi watu wanaona mmeleta mkataba wa hovyo na bado mnatumia nguvu kutuumiza hapana
Bila kujitambua CCM nayo inajitahidi kuamsha watu bila kujua madhara yake.

Sasa hivi kila wanakopita watu wanabaki na maswali ambayo hayajibiki!!! Wangekuwa wanajitambua wangesitisha hiyo wanayoiita elimu
 
Hawaamini kinachotokea, walizoea watanganyika ni wapole sasa wanaona matokeo yake, bandari zetu kwanza.
 
Back
Top Bottom