Wamejenga ukumbi wa kufanya sherehe tunapokaa. Weekend hatulali

Stroke

JF-Expert Member
Joined
Feb 17, 2012
Posts
37,630
Reaction score
47,434
Amani imetoweka kabisa.

Mita chache toka napokaa wamejenga ukumbi wa kufanya sherehe yaani ikifika ile jumamosi basi amani inatoweka ni kelele mtindo mmoja.

Huyu mama wa serikali za mitaa nilikua namheshimu sana lakini kwakweli amenikera kuendekeza hili jambo.

Hatulali makelele mtindo mmoja wakishamaliza mambo yao saa tisa ndio usingizi unakuja.
 
Pole sana
 
Huyo ni mlipa Kodi na ana TIN muulize mwenye nyumba kama kodi unayolipa anakatwa VAT. Ukishindwa Hama mtaa
 
Sorry to say that ,hapo shida ni nyinyi kukaa Maeneo ya "SKWATA" ambapo hakujapangwa hata huyo mwenye bar/ukumbi na yeye ana haki ya kufanya biashara hapo kwenye skwata ,mngejenga sehemu iliyopimwa it means sehemu ya club ingejitenga na makazi.
 
Huyo ni mlipa Kodi na ana TIN muulize mwenye nyumba kama kodi unayolipa anakatwa VAT. Ukishindwa Hama mtaa
Sheria airuhusu kujenga shughuli za starehe kwenye makazi ya watu.
 
Mataga mmekuwa walalamishi sana
 
Sorry to say that ,hapo shida ni nyinyi kukaa Maeneo ya "SKWATA" ambapo hakujapangwa hata huyo mwenye bar/ukumbi na yeye ana haki ya kufanya biashara hapo kwenye skwata ,mngejenga sehemu iliyopimwa it means sehemu ya club ingejitenga na makazi.
Sio kwata mkuu,

Pote pamepimwa.

Eneo lilikua nyumba ya mtu wamefanyia marekebisho tu.
 
Ripoti ofisi za mazingira waruke nao maana anapaswa kuweka sound proof. Usihangaike na hao ofisi za serikali ya mtaa maana wapo kwenye payroll ya mwenye ukumbi kwanza hawanza vifaa vya kupimia ukubwa wa aauti inayoruhusiwa kutoka nje ambayo haitakuwa kero kwenu.

Mstue mtu wa mazingira kwanza hiyo ni deal kwao.
 
Hapo awali yalikuwa makazi binafsi.
Sawa atakuwa kabadilisha ndio maana anatamba kwa kulipa kodi wewe huna guts za kumhoji alitakiwa mwenye nyumba wako ahoji nae ataulizwa una wapangaji je unalipa kodi serikalini? Ndio maana kachagua kuchutama maisha ya songe vumilia au hama mtaa.
 
Sorry to say that ,hapo shida ni nyinyi kukaa Maeneo ya "SKWATA" ambapo hakujapangwa hata huyo mwenye bar/ukumbi na yeye ana haki ya kufanya biashara hapo kwenye skwata ,mngejenga sehemu iliyopimwa it means sehemu ya club ingejitenga na makazi.
Mbezi beach,Masaki,Mikocheni kumejaa mabaa yanapiga kelele sana Napo ni skwata? Yaani siku hizi mitaa ya kishua ndio ina vurugu usiku kuliko uswazi.
 
Watakuwa ma chadema[emoji1]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…