Mkuu, hili jukwaa lina watu wenye akili na elimu zao, kwa hiyo usidhani hatufuatilii mtiririko wa unayobandika humu.
Ulianza kwa hoja ya kuwa Simba wamekopa magari. Hii ya pili ghafla imebadilika, sio kukopa tena, bali kuhoji hela za mikataba zinazoingia katika klabu ya Simba kwamba zinaenda wapi
Mimi nilidhani kwamba ungeendelea na msimamo wako kuwa Simba wamekopa magari ungeonekana kidogo kwamba kuna hoja unasimamia. Kitendo cha kuanza na hoja mpya ya mapato ya mikataba kinaiua hoja yako ya kukopa magari, maana haiwezekani mtu akukopeshe magari halafu akupe na hela!
Endelea na hoja moja walau uonekane ulipitapita shule kidogo, vinginevyo utaonekana kuwa ni mweupe kichwani